MWIGULU AMJIA JUU WARIOBA, ASEMA WAKATI WAKE UMEKWISHA AACHE WATU WAFANYE KAZI, WAZEE WA AINA HIYO WASIENZIEWE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mwigulu-amjia-juu-warioba-asema-wakati.html
Naibu
katibu mkuu wa CCM Mwiguru Nchemba akipokelewa wilayani Gairo
alipokwenda jana kwa ziara yake ya siku moja wilayani humo.
Nchemba akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Gairo.
Nchemba
alipowasili katika ofisi ya CCM wilaya ya Gairo ambapo alikutana na
kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya mkutano wa hadhara.
Mkuu wa wilaya ya Gairo Khanifa karamagi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ialani kwa Nchemba katika kikao cha kamati ya siasa.
Nchemba wakati akielekea katika mkutano wa hadhara
Nchemba akisalimiana na wananchi wa Gairo waliofurika katika mkutano huo
Mwiguru akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akizungumza kabla ya kumkaribisha mwiguru katika mkutano wa hadhara Gairo.
Awali Mwiguru alipowasili katika ofisi za CCM akivalishwa skafu.
habari zaidi soma hapa
NAIBU
katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Mwiguru Nchemba amesema wazee
wanaofuta misingi ya kudumisha amani na utulivu wanchi alioacha Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere wataheshimiwa na kuenziwa na chama hicho na
kwamba wale wanaokiuka wabezwe kwani hawana nia njema na nchi.
Mwiguru
ambaye pia ni naibu waziri wa fedha alisema hayo jana wakati wa ziara
yake wilayani Gairo ambapo alifanya mkutano wa hadhara kuzungumzia kero
kubwa ya maji inayokabili wilaya hiyo.
‘’
Wazee wote ambao wanafuata misingi ya baba wa taifa kudumisha amani na
utulivu wan chi CCM itawaheshimu na kuwaenzi, lakini wale ambao wakati
baba wa Taifa alikuwepo wakawa wanajificha kwa unafiki wao na sasa
wameona kuwa hayupo wajitokeze na kutaka kuvuruga amanni na utulivu
tulionao hatuwawafumbia macho’’ Alisema
Alitolea
mfano mmoja wa wazee hao ni Jaji Warioba ambaye alipewa heshima ya
kukusanya maoni ya katiba na kazi hiyo alishakamilisha lakini cha
kushangaza bado kila kukicha anakaziania kuwepo kwa Serikali tatu jambo
ambalo kamwe CCM halitakubali.
‘’
Huyo mzee ni waajabu kweli, alipewa kazi ya kusimamia ukusanyaji wa
maoni ya katiba lakini sasa kila kukicha unamwona kwenye vyombo vya
habari akililia serikali tatu, hana nia njema na serikali yetu , msimamo
wa CCM ni serikali mbili tuu’’ alisema
Aliwataka
vijana kutambua kuwa serikali tatu ni mzigo ambao haubebeki na kwamba
watakaoumia ni watanzania kwa kuongezewa kodi mara dufu ya hivi sasa.
‘’
Kwa sasa tunahangaika kutafuta ajira kwa vijana, hizo fedha za
kuendeshea serikali tatu badala ziende kwenye mambo ya maendeleo na ili vijana waweze kupata ajira ‘’ alisema
Alisema kuwa kwa sasa kwa sasa pato la taifa ni tririoni 7.7 na kati ya hizo tririoni 4 zinatumika kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi na zilizobakia ndio fedha za maendeleo.
‘’
Sasa hii serikali ya tatu ikija hizi fedha za maendeleo ndio
ziachuhudumia huko na kwamba fedha za maendeleo tutegemee kwa wafadhili
hiyo inaingia akilini kweli? Alihoji
Hata hivyo alisema watahakikisha inakuwepo sheria itakayosimamia fedha za mfuko wa vijana ambazo zitakuwa zinatoka moja kwa moja badala ya kupitia katika mifumo mingine ambapo mara nyingi imekuwa ikikwamisha.
Alifafanua na kusema upo
utaratibu wa kila halmashauri kutoa fedha za mfuko wa vijana ambao kwa
asilimia kubwa hazifikii walengwa kama ilivyokusudia na kwamba sheria
hiyo itasaidia kubana mfumo huo na hivyo fedha kufikia vijana moja kwa
moja.
Wakati huo huo alisema
NAIBU
waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba ametangaza vita dhidi ya matajiri
wanaokwepa kodi kwa kushirikiana na mawakala na watumishi wa Serikali
na kwamba ameomba kupewa taarifa ili aweze kupambana nao.
Mwiguru
alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani Gairo mkoani Morogoro
alipokwenda kusikiliza kero ya maji kwa wananchi wa wilaya hiyo.
‘’
Tunaingia rasmi kwenye vita ya wakwepa kodi, kama kuna mawakala,
watumishi wanaoshirikiana na matajiri hao tupeni taarifa ili
tuwashughulikie, hatuwezi kuzoza kodi kwa wauza vitumbua huku matajiri
wanakwepa kodi’’ Alisema
Alisema
wanaandaa sheria ya kufuta misamaha kwa ya kodi kwa watu ambao
hawastahili sambamba na kuweka sheria bitakayosimamia kuziba mianya ya
ukwepaji wa kodi.
‘’
Wapo matajiri ambao ikiwekwa kodi wanawatumia wananchi kulalamikia ili
wafutiwe kwa kigezo cha kutokuwa na uwezo, sio watanzania wote hawana
uwezo ambao labda ukiweza kodi kwenye simu washindwe kulipa, mbona milio
ya simu wanakwatwa fedha lakini hawalalamiki , hii tumeshaibaini na
sasa tutaishughulikia’’ Alisema
Hata hivyo alisema kuwa wanaangalia uwezekano wa kupekela sheria ya usimamizi mzuri wa fedha za Serikali .
Kwa
upande mwingine Mwiguru aliwatoa hofu wananchi wa Gairo atahakikisha
wanapatiwa visima vya maji vya muda wakati wakisubiri mradi
mkubwa unaofadhiliwa na benk ya dunia ambao kwa sasa unasuasua kutokana
na kuwepo na maji ya chumvi katika yvanzo vilivyokusudiwa kwaajili ya
mradi huo.
Alisema
kwa sasa amepata taarifa kuna maji yanayotoka katika mto uliopo jirani
na mradi huo na kwa kuaznia watatumia kiasi cha shilingi milioni 300 za
fedha za ndani kupata visima hivyo huku juhudi za kuhakikisha chujio la
kuchuja maji ya chumvi zinaendela kufanyika.
Alisema
tatizo la maji ni ajenda tofauti na inatakiwa kushughulikiwa na kupewa
uzito wa kipekee na kwamba isihusishwe na masuala ya kisiasa kama
ambavyo wapinzani wamekuwa wakitumia mwanya huo kwa sasa.
Alisema
serikali inatambua umuhimu wa maji kwa wananchi wake na ndio maana hata
katika bajeti ya mwaka huu fedha nyingi zimeelkezwa katika miradi ya
maji ili kuhkikisha wananchi wanaondokana na dhana hiyo.