MWENYEKITI WA ASERNAL AWEKA ROHO YA `PAKA` KWA WENGER, ASEMA MFARANSA HUYO ATALETA MAKOMBE MENGI EMIRATES
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mwenyekiti-wa-asernal-aweka-roho-ya.html
Kaaminiwa: Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick (kushoto) anaamini Arsene Wenger atawapatia makombe mengi zaidi.
MWENYEKITI
wa Arsenal, Sir Chips Keswick anaamini kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo,
Mfaransa Asernal Wnger muda si mrefu ataleta makombe mengi Emirates
baada ya kubeba ndoo ya FA.
Muda
wowote kutoka sasa, Asernal wanatarajia kutangaza kuongeza mkataba na
Wenger kwasababu kocha huyo mwenye miaka 64 anajiandaa kwenda Brazil
ambapo atakuwa mchambuzi wa kombe la dunia katika televisheni ya
Ufaransa.
Keswick
alisema : 'nina matumaini kuwa ataendelea kufanikiwa zaidi na mafanikio
yanakuja siku si nyingi. Tumeongeza kombe moja na tunahitaji mengine
zaidi"
'Mtu anayefanya kazi kama yeye,
anastahili mafanikio yote yanayokuja katika njia zake. Amefanikiwa na
kamwe sijawahi kuona mtu kama yeye,' aliongeza Keswick kwenye mtandao
wa klabu.
Wenger
ameahidiwa paundi milioni 100 ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania taji la ligi kuu soka nchini England msimu ujao.