MCHUNGAJI APATWA NA GONJWA LA AJABU WATOTO WAKE WAMTENGA
Mchungaji Mary Izengo.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mchungaji-apatwa-na-gonjwa-la-ajabu.html
Mchungaji Mary Izengo.
MARY Izengo (52), mkazi wa Kijiji cha Umanda- Msalala, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza anateseka kiasi cha kutamani afe kufuatia gonjwa la ajabu alilonalo huku akisema ndugu, wakiwemo watoto wake wamemtenga.
Akizungumza
na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Wadi Namba 23, Jengo la
Sewa Haji kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwanamke huyo alisema
usiombe gonjwa hilo likupate kwani ugonjwa unaomkabili ni wa uvimbe
mkubwa usoni ambapo unamtesa kwa kipindi kirefu huku akionekana kero
kubwa katika jamii.
ATOA HISTORIA YAKE HUKU AKILIA
Hata
hivyo, mwanamke huyo ambaye wakati akizungumza na Uwazi mara kwa mara
alikuwa akilia, alisema:“Nilizaliwa mwaka 1962 katika Kijiji cha Umanda
Msalala, wilayani Sengerema nikiwa mzima wa afya wala sikutegemea kama
siku moja ningekuja kuwa katika hali hii.
“Nikiwa
na umri wa miaka mitano ndipo nilipoanzwa na tatizo hili. Ulianza kwa
kutoka vipele vidogovidogo mdomoni ambavyo viliniletea maumivu makali.
Wazazi walinipeleka hospitali nikatibiwa kwa kuchomwa sindano lakini
bila mafanikio.
“Hali
ilipozidi kuwa mbaya, wazazi hawakukata tamaa, wakanipeleka Hospitali ya
Wilaya ya Sengerema, lakini nako pia ikashindikana, nikarudishwa
nyumbani.
“Hali
yangu iliendelea kuwa mbaya zaidi nikachangiwa fedha na kupelekwa
Hospitali ya Bugando, Mwanza ikashindikana pia, nikarudishwa tena
nyumbani.
“Kwa
bahati nzuri, alijitokeza mwanaume na kunioa akisema hatajali ugonjwa
wangu na baadaye wazazi wangu walifariki dunia,” alisema mwanamke huyo
akiendelea kulia.
Akaendelea:
“Nilizaa watoto wawili kwa mume wangu na alinipenda sana na kunisaidia
kwa kadiri ilivyoweza kutokana na kipato chake. Alikuwa mkulima wa jembe
la mkono.
“Ila
baadhi ya ndugu zake walipoona sura yangu inazidi kubadilika walimshauri
anifukuze eti ili ugonjwa wangu usije ukaenea katika ukoo lakini
aliwakatalia na kuzidisha mapenzi kwangu jambo ambalo lilinitia moyo.
“Mwaka
2011 mume wangu alifariki dunia na kuniachia watoto. Nililia sana kwani
nilijua nitateseka kupita kawaida. Baada ya baba yako kufa, watoto nao
wakanikimbia wakisema ugonjwa wangu ni uchuro.
“Nikawa
naishi peke yangu. Mara nyingi nilikuwa nikishinda njaa kama majirani
hawakuniletea chakula, nilitamani kujiua na nikasema bora nife tu.
AENDA MKUTANO WA MBUNGE, APATA MSAADA
Mary
aliendelea kusema kuwa, siku moja alijikuta akisukumwa kwenda kwenye
mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Nyang’wale wilayani Geita, Mhe. Ahmed
Nassor Amar ‘Gulamali’.
“Haikuwa
kawaida yangu kushiriki mikutano, lakini siku hiyo nilikwenda. Mwisho wa
mkutano, mbunge aliniona akanihurumia sana na kuniambia nije Muhimbili
nipatiwe matibabu, akanipa shilingi laki tatu.
“Ndipo
Aprili mwaka huu nikamtafuta msamaria mwema, akanileta hapa Muhimbili
ambapo madaktari wamenipokea vizuri sana,” alisema mama huyo.
“Madaktari
walinifanyia uchunguzi na wakanieleza kwamba kuna mshipa unapitisha
damu kwa wingi ndiyo maana nimevimba hivi, wakasema matibabu yake hapa
nchini haiwezekani mpaka India. Kwa hiyo kwa sasa nasubiri kama nitaweza
kwenda huko.
ASHANGAZWA NA NDUGU
“Kinachonishangaza
na kunisikitisha ni kwamba, hapa Dar es Salaam nina kaka yangu,
nilipofika tu hapa hospitali nilimuomba muuguzi simu nikampigia
kumjulisha kuwa naumwa nipo Muhimbili. Miaka mingi hatujaonana akafikiri
kuwa ugonjwa wangu ni wa kawaida.
“Alipokuja na kuniona alitokwa machozi na kuondoka. Kuanzia hapo kila nikimpigia simu hapokei,” alisema mama huyo.
Mary
anaomba msaada ili aweze kupata fedha zitakazomuwezesha kwenda India
kutibiwa. Ukitaka kumsaidia tuma fedha kwa namba 0683 406 680 ya afisa
ustawi wa jamii aliye karibu naye.