MBEYA CITY FC YAANGUKIA KUNDI LA KIFO CECAFA NILE BASIN, MWAMBUSI APANGA MAJESHI YAKE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mbeya-city-fc-yaangukia-kundi-la-kifo.html
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc
imepangwa kundi B katika michuano mipya ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika
Mashariki na Kati (CECAFA) ijulikanayo kwa
jina la `CECAFA Nile Basin` inayotarajia kushika kasi kuanzia mei 22 hadi juni
4 mwaka huu nchini Sudan ikijumuisha timu 16.
Katika droo ya michuano hiyo iliyopangwa leo,
Mbeya City imepangwa na timu za AFC
Leopards ya Kenya), El Merreikh Al Fasher ya Sudan na Elman ya
Somalia.
Kundi A: El Merreikh ya Sudan, Victoria
University ya Uganda, Malakia ya Sudan Kusini na Polisi ya Zanzibar.
Kundi: Al
Ahli Shandi ya Sudan, Al Masry ya Misri, Defence ya Ethiopia na Dkhill
ya Djibouti.
Kundi D: Hey Al Arab ya Sudan, Arab Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
Kundi D: Hey Al Arab ya Sudan, Arab Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
Mbeya City fc wamepata nafasi ya kushiriki
michuano hii baada ya mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kujiondoa.
Uongozi wa Mberya City kupitia kwa mwenyekiti wake
Mussa Mapunda umesema nafasi hii ni adimu , hivyo watahakikisha wanajiandaa vizuri ili
kuiwakilisha vizuri Tanzania.
Mapunda alisema nguvu waliyokuwa nayo katika
michuano ya ligi kuu ndio wanaipeleka Sudan na tayari wachezaji waliopo Mbeya wameanza
mazoezi , wengine walikuwa nje ya jiji
hilo wakiendelea kuripoti.
Kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi kwa upande
wake amefurahishwa na kupata ratiba mapema, hivyo anaanza kusuka kikosi chake
mapema.
Mwambusi aliyeiongoza Mbeya City fc kushika nafasi
ya tatu msimu uliopita anatarajia kuwadhihirishia watanzania kuwa klabu hiyo si
ya kubeza.
Kwa mara ya kwanza, Mbeya City mwanzoni mwa mwaka
huu walishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayoshirikisha klabu kutoka
nchi za Afrika Mashariki, lakini walitolewa mapema na waliporudi ligi kuu
waliendeleza kasi yao.
Hii itakuwa mara ya pili kushiriki michuano
inayoshirikisha timu za nje ya nchi kama ilivyokuwa kwa michuano ya Mapinduzi,
hivyo wapenzi wa soka nchini Tanzania wana hamu ya kuiona Mbeya Cuty ikifanya
vizuri.