MAPENZI YA ROONEY KWA KAI USIPIME, AMPIGA BONGE LA BUSU WAKATI WA MAZOEZI YA ENGLAND
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mapenzi-ya-rooney-kwa-kai-usipime.html

Mapenzi: Wayne Rooney (kulia) akimbusu mwanaye Kai kabla ya mazoezi ya Englan.
Wayne
Rooney alionesha mapenzi makubwa kwa mtoto wake wa kiume anayejulikana
kwa jina la Kai baada ya kumbusu muda mfupi kabla ya kujiunga na wenzake
katika mazoezi ya timu ya taifa ya England nchini Ureno.
Mshambuliaji huyo wa
Manchester United alionekana mwenye furaha na morali kubwa wakati alipombeba mwanaye aliyemkimbilia kabla ya kuanza mazoezi.
Rooney
kwa haraka alimbeba Kai aliyeonekana amevaa jezi za England na kumrusha
hewani kwa mapenzi ya dhat kabisa kabla ya kuanza programu ya mazoezi
na Roy Hodgson.

Mtu wa furaha: Rooney akitabasamu baada ya mtoto wake Kai kumkimbilia

Wametulia: Rooney na Steven Gerrard wakibadilishana mawazo wakati wa mazoezi ya England

Wapendanao: Rooney
alisafiri na familia yake kupunga upepo nchini Ureno, huku akiwa pamoja
na timu ya taifa ya England katika kambi ya maandalizi ya kombe la dunia