HAYA SASA FID Q NA DAYNA WAINGIA KATIKA MKANGANYIKO, FID Q AMCHANA LIVE, MKOROGO NAO WAHUSIKA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/haya-sasa-fid-q-na-dayna-waingia-katika.html
“Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Soudy brown kamtafuta Fid Q ambapo
alipoulizwa kuhusu hili majibu yake alidai kuwa katika ngoma hiyo
hamzungumzii Dayna Msanii bali anamzungumzia Dayna msichana anayeishi
nae kitaani maeneo ya Mikocheni kwa Nyerere.
Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi
sasa hivi amejichubua ngozi yake na kuwa mweupe ambapo baadae Fid Q
aliuchambua kiutaalam mstari huo na kusema kuwa wadada wanaofanya hivyo
wanaua melanie.
Ambacho ni kitu muhimu sana kwenye
ngozi na hupatikana zaidi kwenye ngozi nyeusi ya kiafrika chembechembe
ambazo huilinda ngozi isiunguzwe na jua.
Majibu ya Dayna baada ya kupigiwa
simu na Soudy Brown kutaka kujua kama ameshaisikia hiyo line ya Fid Q
alichokijibu ni ameisikia na anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa
wakati huu amepunguza kidogo kutumia mikorogo.