MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MANDERA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mama-salma-kikwete-atembelea-shule-ya.html
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi mara baada ya kuwasili kwenye Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani bagamoyo tarehe
10.5.2014.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy
akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye
shule hiyo tarehe 10.5.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia jaribio la somo la Fizikia
(Hooke’s Law: Inayosema ‘The force needed to extend or compress a spring
by some distance is proportional to that distance’) lililokuwa
likifanywa na mwanafunzi Mwajuma Mwanankuta wa Kidato cha 4 katika Shule
ya Sekondari ya wasichana ya Mandera tarehe 10.5.2014.Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko
Wilayani Bagamoyo wakiimba wimbo wa shule kwa ajili ya kumkariisha Mlezi
wa shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shule hiyo tarehe
10.5.2014.Mke
wa Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko
wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete akizungumza na
wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
shule tarehe 10.5.2014.Daktari
Hadija Mwamtemi aliyefuatana na Mama Salma Kikwete anaonekana
akimhudumia mwanafunzi (jina lake halikuweza kupatikana) wa Shule ya
Sekondari ya wasichana ya Mandera aliyekuwa mgonjwa wakati Mama Salma
alipotembelea shuleni hapo tarehe 10.5.2014.