Flatnews

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. MUHONGO MAKADIRIO YA BAJETI 2014/2015




: Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof S.Mhongo, Makadirio ya Bajeti 2014/2015

Karibuni kwa Live Updates ya Hotuba Hii

 * Anasema kuwa Wizara ilitengewa Trion1.3 kwenye bajeti iliyomalizika. Hadi sasa, imepokea jumla ya shilingi bilioni 660
*Wizara imepata hati safi isiyo na mashaka kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za Umma
*Wizara imepanga kukusanya jumla ya shilingi bilioni240.59 kupitia vyanzo vyake
*kuhusu uzalishaji umeme, anasema kuwa 2013 hapakuwa na mgawo wa umeme kama ilivyotangazwa. Amesema kuwa mgawo uliokuwepo ni wa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye magazeti
*Anasema kuwa uzalishaji wa umeme umeongzeka kutoka MW 891 mwaka 2005 hadi kufikia MW 1585 mwaka 2013
*Mradi wa kuzalisha umeme wa MW 600 huko Mtwara, upembuzi yakinifu utakamilika Julai mwaka huu
*Serikali imeanza mchakato wa kusafirisha umeme wa KV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga, mradi utakamilika mwaka 2015 na Bilioni 2.5 zimepangwa kuanza kuutekeleza
*Mradi wa kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea utaanza kutekelezwa na jumla ya bilioni 16 zimetengwa
Mradi wa kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi hadi Arusha, Mradi utakamilika mwaka 2017
* Upanuzi wa wa njia ya umeme toka Tunduma hadi Nakonde, Zambia kv 33, jumla ya bilioni sita zimetengwa
*Mradi wa kusambaza umeme kwenye mikoa ya kanda ya Ziwa, Njiro Arusha na DSM, jumla ya bilioni Sita zimetengwa na utakamilika mwaka ujao
*Mradi wa kuimarisha mfumo wa usambazaji umeme DSM utaanza kutekelezwa mwaka huu. Bilioni moja zimetengwa na jumla ya fedha zinazohitajika ni bilioni 123

MIRADI YA TANESCO NA REA
*Kiwango cha waliounganishwa umeme vijijini kimeongezeka kutoka asilimia tano hadi saba
*Wizara imefanikiwa kufikia lengo la CCM la kufikia asilimia saba
*Gharama za kuunganisha umeme vijijini ni 27,000 tu

MIRADI YA UMEME YA LINDI NA MTWARA
*Wizara inatekeleza miradi 52 ya umeme mikoa ya Lindi na Mtwara
*Gharama ya kuunganisha umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni 99,000

MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA
* Utandazaji wa bomba la gesi toka Mtwara hadi Lindi umefikia 78%
*Mradi wa kutandaza bomba utakamilika Julai 2014

NISHATI YA MAFUTA
*Kampuni ya Oman Trading International ilishinda zabuni ya kuiuzia TPDC na imekubali kuuza kwa mkopo mafuta hayo

SERA YA UWEZESHAJI WA WAZAWA(LOCAL CONTENT)
* Sera itakamilika Desemba 2014. Kukamilika kwake kutawawezesha wananchi kuwekeza kwenye nishati ya gesi na mafuta
* Rasimu ya sera imesambazwa kwa wadau

MADINI

WACHIMBAJI WADOGO
*Jumla ya shilingi milioni 88 wamepewa kama ruzuku wachimbaji wadogo kwenye vikundi 11. Julma ya shilingi Bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo kwa mwaka ujao. Vikundi hivi 11 pia vitapewa ruzuku ya dola 50,000 kama ruzuku kabla ya kumalizika mwaka huu wa fedha
*Jumla ya kilometa za mraba zaidi ya 2000 zimetengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo
* Watanzania wanamiliki asilimia sabini ya Leseni za Madini

STAMICO
* Jumla ya watumishi wapya 78 waliajiriwa kwa mwaka huu wa fedha unaomalizika. Lengo ni kukiimarisha kitengo

WAKALA WA JIOLOJIA
*Wakala umeendelea kufanya utafiti mbalimbali
Wakala utachora ramani nne za jiolojia kwenye mikoa ya Ruangwa, Nachingwea, Kilwa na Liwale

RASILIMALI WATU
*Wizara imeajiri watu,ishi wapya 227
*watumishi 214 wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
* Wizara imeendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali, taasisi na mashirika ya kimataifa

SHUKRANI
*ametoa shukrani kwa manaibu Waziri, Katibu Mkuu, Eliakimu Maswi, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi nk. Pia amemshukuru aliyekuwa Naibu waziri George Simbachawene kwa utendaji uliotukuka

KAULI MBIU
*Ametoa kaulimbiu ya Wizara kuwa ni HAKUNA KUSHINDWA HAKUNA KUKATA TAMAA

MAOMBI YA FEDHA
*Wizara iinaomba fedha Jumla ya Shilingi 1,8,255,652,000

Post a Comment

emo-but-icon

item