EDEN HAZARD ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA CHELSEA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/eden-hazard-abeba-tuzo-ya-mwanasoka.html
Nyota: Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho akimpa
zawadia Eden Hazard baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka
Kipenzi cha mashabiki: Hazard aliifungia Chelsea
mabao 14 katika michezo ya ligi na kumaliza katika nafasi ya tatu.
EDEN Hazard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
mwaka wa Chelsea katika msimu wake wa pili klabuni hapo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amefurahia
mafanikio ya msimu huu chini ya kocha Jose Mourinho na kufanikiwa kufunga mabao
14 katika michezo yote ya ligi kuu na kumaliza akiwa mfungaji bora wa klabu.
Hazard aliyejiunga na Chelsea majira ya
kiangazi mwaka 2012 akitokea klabu ya Lille ya Ufaransa, mwezi uliopita
alishinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora kijana wa mwaka na alishika nafasi ya
pili nyuma ya Luis Suarez wa Liverpool katika tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka
nchini England.
Hazard alisema: 'Nataka kusema asante sana"
"Wenzangu watatu waliotajwa walistahili tuzo
hii. Tunafahamu tulicheza kwa ushirikiano, lakini tuzo binafsi wakati fulani ni
nzuri, kwahiyo nitaichukua tuzo hii mpaka nyumbani kwangu na kufurahia pamoja
na familia yangu"