https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/brendan-rodgers-asema-ataongeza-majembe.html
Mipango inaendelea: Brendan Rodgers tayari ameshaanza kuwaza namna ya kuiboresha Liverpool msimu ujao.
KOCHA wa Liverpool,
Brendan Rodgers ameumia sana baada ya kikosi chake kushika nafasi ya
pili katika mbio za ubingwa wa ligi kuu soka nchini England, lakini
amesisitiza kuwa timu yake itarejea kushindana tena msimu ujao.
Mabao
ya Daniel
Agger na Daniel Sturridge yaliipa ushindi wa mabao 2-1 Liverpool dhidi
ya Newcastle, lakini bao la wapinzani hao wa majogoo wa jiji lilitokana
na Martin Skrtel kujifunga mwenyewe na likiwa ni bao la nne la
kujifunga msimu huu.
Licha
ya Liverpool kushinda, Anfield ilikuwa kimya baada ya Man City kushinda
mabao 2-0 dhidi ya West Ham na kutwaa ubingwa wa pili ndani ya misimu
mitatu.
Rodgers aliwaambia Sky Sports: 'Tulicheza vizuri sana lakini hatukuweza kupata matokeo ya kuridhisha".
"Wachezaji wamekuwa katika kiwango cha
juu, kushinda mechi 12 kati ya 14 inaonesha kuwa klabu ina kundi la watu
linaloweza kufanya vizuri msimu ujao. Tutajifunza kwa kila kosa
tulilofanya msimu huu na kujiandaa kwa msimu ujao".
Alipoulizwa kama klabu yake inaweza
kupambana kwa kasi ile ile msimu ujao, Rodgers alisema: "Ndiyo.
Tumeshika nafasi ya pili mbele ya timu imara. Hongera kwa Manchester
City, wameshinda taji wakiwa na kocha mzuri na kikosi cha wachezajii
bora duniani, nawapongeza sana".
"Tumepambana mpaka mchezo wa mwisho. Hii ni timu iliyoshika nafasi ya sabu mwaka jana.
"Tunajua tutakuwa bora zaidi kwasababu tutaboresha kikosi na tutaendelea kujiimarisha zaidi".
Tumekomaa sana: Rodgers amafurahi kwasababu wachezaji wake wamepambana na Man City mpaka mechi ya mwisho