Balozi wa Finland Nchini Sinikka Antila akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kuwasili.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akisisitiza jambo katika kikao hicho. Kati ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Finland katika masuala ya teknolojia, uendelezaji wa rasilimaliwatu na usimamizi wa fedha
Balozi
wa Finland Nchini Sinikka Antila (kulia) akizungumzia jinsi nchi ya
Finland ilivyopiga hatua kimaendeleo hususani katika sekta ya nishati
pamoja na utayari wa nchi hiyo kushirikiana na nchi ya Tanzania katika
kuimarisha sekta za nishati na madini.