ANDIKENI HABARI ZA KUMKOMBOA MWANANCHI : JAJI BOMANI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/andikeni-habari-za-kumkomboa-mwananchi.html
Mshehereshaji
ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha
baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi
Jaji Mstaafu Mark Bomani.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Mwandishi wetu
Jaji
Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha
kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote
itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia
maendeleo mwananchi kwa haraka.
Akitoa
risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji
Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la mwanahabari ni kuwaelimisha
baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao hawana uelewa mkubwa
na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo ambayo
yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi
na kejeli.
Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
“Zoezi
la mchakato wa Katiba ni kubwa na wabunge wengi wa Bunge Maalum la
Katiba hawaelewi wajibu wao katika kuijadili Katiba hiyo matokeo yake
ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
Mara
nyingi Watanzania wameshuhudia mijadala ya kejeli, malumbano, matusi,
kudharauliana pale hoja zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na
upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na
imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
Jukumu
la wanahabari ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba
Mpya na kuandika habari za maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe
endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha
maisha yao.
Meza
Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly,
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest
Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji
Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais
wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth
Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), Bw. John Mirenyi.
“Inasikitisha
kuona kuwa hali ya Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale
katika sehemu nyingi hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita
kwa kukosa fursa muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”,
amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Wakati
huo huo mgeni huyo rasmi amekemea tabia ya kuandika habari za kuwasifu
viongozi na kupokea Rushwa hali iliyojitokeza katika miaka ya hivi
karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa tasnia ya habari kutofuata
maadili ya uandishi.
Amesema
kwamba nchi itaendeshwa kwa kusimamia haki na ukweli na kuwataka
wanahabari wasichoke kuisimamia haki na uhuru wa nchi yao bila woga
kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
Mgeni
rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
“Kuna
tabia ya vyombo vya habari ya vyombo vya habari kununuliwa ili
visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani vyombo vya habari ni kioo
cha jamii”.
Akizungumzia
kuhusu sheria za habari za mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni
aibu kuona mswaada wa sheria ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10
kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
Amewataka
waandishi wa habari wasikate tamaa na badala yake waendelea na
kupambana kuhakikisha kwamba harakati za kupata Sheria ya Haki ya Kujua
inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso, kupigwa, kuteswa,
kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
“Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani.
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Habari wakisikiliza risala ya mgeni rasmi.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa wa Arusha kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani yaliyofanyika jijini Arusha kenye ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa AICC.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania
(MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, akizungumza kwenye maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye
ukumbi wamikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Wageni waalikwa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa kwenye ukimya kumkumbuka Mwandishi aliyeuwawa mkoani Iringa Daudi Mwangosi.
Mkurugenzi
wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa
(UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas
kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
Meneja
Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), Bw. John Mirenyi, akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali
yaliyoandaliwa na baraza hilo yakiwemo yenye madhila mbalimbali yaliwahi
kuwakumba baadhi ya waandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura,
akizungumzia mchango wa mfuko huo unaowawezesha waandishi wa habari
kutafuta habari za uchunguzi na zinazoigusa jamii.
Wasanii
wa Bendi ya Mrisho Mpoto (Mjomba Band) wakitoa burudani kwa wageni
waalikwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa juma.
Sehemu ya wadau wa tasnia ya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo.
Katibu
wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry
Muhanika, akisoma hotuba kwa niaba ya Dr. Reginald Mengi kwenye
maadhisho hayo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akizungumzia wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akizungumzia changamoto
mbalimbali zinazowakumba waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi
wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka, akizungumzia changamoto za usawa wa
Kijinsia katika uongozi kwenye Vyombo vya Habari nchini.
Meneja
Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, akizungumzia ushiriki wao kwenye
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 ambapo aliwataka
waandishi wahabari kutumia kalamu zao vizuri katika kukuza Utalii wa
Tanzania ndani na nje ya nchi.
Meneja
Uhusiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bw. Adam Akyoo, akifafanua
jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani 2014 ambapo amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao
katika kupambana na suala la Ujangili linaloendelea nchini.
Mrisho
Mpoto akiwafungua vitambaa wasaani wa Mjomba Bendi kama ishara ya
kuwapa Uhuru waandishi wa Habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni
rasmi kama ujumbe wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014.
Mrisho
Mpoto na Bendi yake akighani mashairi na kuelezea madhila wayapatayo
waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za
kila siku.
Makamu
wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC),
Jane Mihanji akimkaribisha mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani kuzindua
Video mpya ya wimbo “Uhuru Wangu” wa Mrisho Mpoto uliokuwa kwenye
Albamu yake mpya inayoitwa WAITE.