WAZIRI PROF. MAKAME MBARAWA ASHUHUDIA MAKAMPUNI YA SIMU YAKIWEKA SAINI MKATABA WA MAKABALIANO YA USAMBAZAJI HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI KUPITIA RUZUKU YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/waziri-prof-makame-mbarawa-ashuhudia.html
001:
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa
(kushoto) akimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano
wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (kulia) muda mfupi kabla ya
kuanza kwa hafla ya utiaji saini mikataba ya usambazaji huduma za
mawasiliano ya simu za mkononi maeneo ya vijijini kati ya makampuni ya
simu na Mfuko wa Wamasiliano kwa Wote - (UCSAF) jijini Dar es salaam.
Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilano wa Airtel Beatrice Singano.
Mkuu
wa Idara ya Sheria wa Vodacom Ngayama Matongo akimuongoza Ofisa Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Georgia Mutagahywa (aliyeketi)
kutia saini mkataba wa makabaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano
vijijini kupitia ruzuku ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye
hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Wa pili kulia aliyesimama ni
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa
akishuhudia. Vodacom kupitia mfuko huo itafikisha huduma kwenye kata 37
za pembezoni mwa miji na yenywe ikiahidi kufikisha huduma kwenye kata 36
za pembezoni kwa gharama zake ili kuwawezesha watanzania wasihia
vijijini kuunganishwa kwenye mtandao wa huduma za simu za mkononi.
Kutoka
kulia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia
Mutagahywa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga
wakitia saini makubaliano yanayayawezesha makampuni ya simu kupokea
ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo pemebezoni na
miji kadiri walivyoomba. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye
kata 73 kati ya hizo 37 kupitia ruzuku YA UCSAF.
Ofisa
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa kulia
akibadilishana nyaraka za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL
Kamugisha Kazaura zinazohusiha upokeaji wa ruzuku kwa ajili ya kufikisha
huduma za mawasiliano vijijini inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote (UCSAF).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter
Ulanga akisainia makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma
kwenye kata 73 zilizopo vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku hiyo. Wa
pili kulia waliosimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof Makame Mbarawa.