RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU 2,181 KWA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/rais-kikwete-akabidhi-vitabu-2181-kwa.html
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi
vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo
vya Jeshi ili kuongeza taaluma.
Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya
kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo
Monduli, Mkoani Arusha.
Library hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.
"Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi
nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu
ya Monduli”.
Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange
amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania
kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.
“Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na
kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia
sana mafanikio haya” amesema Jenerali Mwamunyange .
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Aprili,2014

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi vitabu 2181 kwa uongozi
wa Jeshi(JWTZ) kwa matumizi katika maktaba mablimbali za jeshi
nchini.Wapili kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na
Watatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu Jeshini Luteni Jenerali Samuel Ndomba.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi na makamanda
waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi
vitabu 2181 kwa ajili ya matumizi katika maktaba za jeshi.Vitabu hivyo
ni mchango binafsi wa Rais Katika kuboresha mafunzo ya kisasa jeshini,
(picha na Freddy Maro)
