NAPOLI, SABELLA `WAPANIKI` KUUMIA KWA HIGUAIN
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/napoli-sabella-wapaniki-kuumia-kwa.html
KLABU
ya Napoli imekumbwa na wasiwasi mkubwa baada ya kuumia kwa Gonzalo
Higuain katika mechi yao na Inter Milan hapo jana uwanja wa San Siro
iliyomalizika kwa suluhu (0-0).
Mshambuliaji
huyo raia wa Argentina alilazimika kutoka katika mchezo huo wa Seria A
baada ya kugongana na beki wa Inter, marco Andreolli.
Napoli
wamethibitisha leo hii kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid
amepata majeruhi ya kifundo cha mguu na kuwa hatarini kukosa mechi ya
Coppa Italia wiki ijayo.
“Majibu
hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa na madaktari wa klabu juu ya
hali ya Gonzalo Higuain baada ya kugongana na Andreolli kwenye mechi ya
Inter dhidi ya Napoli”.
“Higuain hayuko katika hali nzuri na tathmini zaidi ya afya yake itatolewa siku zijazo”.
Kocha
wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabella amesitushwa na
majeruhi ya Higuain na anaomba apone haraka kwasababu ni moja ya
washambuliaji atakaowatumia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye miaka 26 mpaka sasa amefunga mabao 24 katika mechi 44
alizocheza tangu ajiunge na Napoli mwezi wa nane mwaka jana kwa uhamisho
wa paundi milioni 40 kutoka Real Madrid.
