MHOLANZI VAN GAAL AMBAKISHA RVP MAN UNITED
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/mholanzi-van-gaal-ambakisha-rvp-man.html
HALI
shwari sasa!. Mshambuliaji wa Manchester United, Mholanzi, Robin Van
Persie ameamua kuendelea kukaa katika klabu hiyo kufuatia kufukuzwa kwa
David Moyes.
Kilichomvutia zaidi
nyota huyo ni klabu hiyo ya Old Trafford kutaka kumleta Mholanzi
mwenzake, Louis Van Gaal kurithi mikoba ya ukocha mkuu.
Taarifa
za kuaminika zinaeleza kuwa Van Gaal tayari ameshakubali vipengele vya
mkataba saa 48 zilizopita ili kuwa kocha wa kudumu wa Man united.
Sio
siri kuwa Van Persie amekuwa na mahusiano mazuri na kocha wake wa timu
ya taifa na sasa anaona itakuwa jambo zuri kukaa pamoja Old Trafford
baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini
Brazil.
Taarifa
za ndani ni kuwa kocha huyo wa Uholanzi na nahodha wake RVB wanatumia
wakala mmoja, bwana Kees Vos ambaye kwasasa yupo katika vikao vya
makubaliano ya kazi mpya baina ya Van Gaal na Man United.
Van
Persie alikuwa akihusishwa kuihama Man United majira ya kiangazi mwaka
huu kwasababu klabu yake imeshindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa
katika msimu wake wa kwanza ambao alibeba taji chini ya Sir Alex
Ferguson.
Pia
kulikuwa na hali ya kutoelewa na bosi wake David Moyes kwa madai kuwa
mbinu za ufundishaji za Mscotish huyo zilikuwa haziendani na mfumo wa
uchezaji wa Van Persie.
