DIAMOND ANATAFUTWA CHINA.....ALIYEJIFANYA DANSA WAKE ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/diamond-anatafutwa-chinaaliyejifanya.html

STAA wa muziki wa bongo fleva nchini, Abdul Nassib "Diamond" ametakiwa kutokanyaga kabisa nchini China na kwamba akitokeza pua yake nchini humo asahau kabisa kurudi uraiani...
Hiyo
inafuatia kijana mmoja mtanzania kukamatwa wiki iliyopita
uwanja wa ndege wa Macau China na kudai kuwa yeye ni
mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....
Habari
kutoka Macau China zinadai kuwa kijana huyo aliyejulikana kwa
jina moja la Manyota alikamatwa akiwa kwenye harakati za
kuingiza mzigo huo wa dawa za kulevya kwa kupitia uwanja wa
ndege wa Macau....
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, inaarifiwa kuwa Manyota
alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita katika uwanja uleule
aliokamatwa mtanzania mwingine Jackline Patrick, anayesotea
rumande mpaka hii leo huko huko Macau China.