Flatnews

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA MANENO YENYE UJAZO MZITO KATIKA MSIKITI WA NUNGE MJINI DODOMA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.

Ametoa wito huo jana mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma. 

Alisema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati.

“Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

“Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi nyumbani na kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao wawaombee dua wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Novemba Mosi, mwaka huu ili waweze kufaulu.

Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao waendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi.

Aidha, Waziri Mkuu alichangia sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa zahanati katika msikiti huo. Miradi inayojengwa na waumini wa msikiti huo kwa sasa ni zahanati, madarasa ya shule ya awali na shule ya ufundi.

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Hot in weekRecentComments

Recent

Kesi ya Godbless Lema na mkewe kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakwama kusikilizwa..

Kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33), imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali. Hatu...

PICHA 18: Style za nywele za baadhi ya mastaa wa muziki Nigeria

              Mastaa wa muziki ni watu ambao wanapenda kwenda na fashion kuanzia mavazi mpaka style za unyoaji. Kwa upande wa mastaa wa Nigeria tumez...

Donald Trump Akataa Kulipwa Mshahara wa Urais

Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani. Trump ameweka msimamo huo jana katika mahojiano maalum na mtangazaji maa...

Jealousy!!! Justine Skye can't stand seeing Wizkid with other girls

As much as we know, Wizkid and Justice Skye are together. Maybe not a great deal. But, at least, there's something going on with the two. To further prove the possibility of the two being deeply in...

Comments

Anonymous:

Hahahaha Safi sana nidhamu ikae Pahala pake

item