Wandili wa SEMA ajitosa kuwania ubunge jimbo la Singida mjini kwa tiketi ya ACT
Mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la SEMA mkoani Singida, Jeremiah Paul Wandili, (katikati) akitangaza nia ya kugombea u...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/wandili-wa-sema-ajitosa-kuwania-ubunge.html

Mfanyakazi
wa shirika lisilo la kiserikali la SEMA mkoani Singida, Jeremiah Paul
Wandili, (katikati) akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Singida
mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo. Kulia ni Mwakilishi wa mwenyekiti
wa ACT Wazalendo mkoa wa Singida, Peter Mkenyi na kushoto ni Mratibu wa
harakati za Wandili za kugombea jimbo Peter Lisu.(Picha na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
KIJANA
mfanyakazi wa Shirika lisilo la kiserikali la SEMA Singida Mjini,
Jeremiah Paul Wandili (27), amejitosa kuwania nafasi ya ubunge jimbo la
Singida mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo.
Wandili
amedai kuwa yeye ni kijana mwenye nguvu na afya njema na lengo lake kuu
na kiu yake,ni kuona mabadiliko makubwa kwa wananchi wa jimbo la
Singida mjini.
Alizungumza
na waandishi wa habari juzi, Wandili alisema amechukua uamuzi huo
mzito, baada ya kujikagua na kubaini kwamba anao uwezo mzuri wa
kuwatumikia wakazi wa Jimbo la Singida na kudai kwamba kero/
changamoto zinazowakabili wananchi, anazifahamu kwa kina.
Alisema
pia amejitokeza kupitia ACT – wazalendo akiamini ndicho chama pekee
chenye uwezo wa kulivusha jimbo la Singida mjini, katika matatizo
mbalimbali yanayowakabili wananchi na kuleta mabadiliko makubwa mapema
iwezekanavyo.
Akifafanua,
Wandili alisema binafsi yeye anachukizwa na umaskini uliokithiri katika
jimbo la Singida mjini, na endapo Chama chake kitampitisha na kisha
wananchi wakampa ridhaa ya kuwawakilisha, vita dhidi ya umaskini,
itakuwa kipaumbele chake cha kwanza.
“Nina
imani kuwa wananchi wa Jimbo la Singida Mjini, wanauchukia umaskini,
kwa hiyo wote wataniunga mkono katika kukabiliana na umaskini huu ambao
umesababisha washindwe kuishi maisha bora”,alisema.
Alisisitiza,
alisema wananchi wa Jimbo la Singida Mjini hawana budi kuachana na
baadhi ya wanasiasa wanaotumia umaskini wa wananchi kama mtaji wao,
katika kufanikisha malengo yao ya kisiasa.
“Nimeziona
fursa mbalimbali katika jimbo letu ambazo hazijatumiwa ipasavyo, kwa
imani yangu ni kwamba kama fursa hizo zitatumwa vizuri, basi
zitatokomeza umaskini kwa haraka kupitia kwa wananchi wenyewe”,alisema
Wandili.
Alifafanua
zaidi, alisema atatumia mbinu shirikishi katika kuweka miundo mbinu
rafiki itakayochangia ukuaji wa uchumi na kwa kitendo hicho, adui
umaskini atatokomeza kabisa.
“Tunataka
tufungue ukurasa mpya wa siasa hapa jimboni. Tutaanzisha siasa zitakazo
shirikisha masuala ya vijana, wanawake, wazee, wakulima, wafanyakazi,
wajasiriamali, wafanyabiashara na wote wenye mapenzi mema na maendeleo
la jimbo letu, ni lengo kuu liwe ni kutokomeza umaskini”, alisema.