Wakazi wa Dar es salaam kupata matibabu yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitali za Apollo
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/wakazi-wa-dar-es-salaam-kupata-matibabu.html

Watanzania
wanashauriwa kuitumia fursa hii ya kipekee ya ziara ya kitabibu
itakayofanywa na madaktari kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad. Kwa
miaka mingi, watanzania wameshindwa kupata matibabu sahihi nchini
kitendo ambacho kimewasababishia kusafiri nje ya nchi kupata matibabu
sahihi ya mfumo wa fahamu, uti wa mgongo, figo pamoja na magonjwa
yanayohusiana na mfumo wa mkojo. Nia na madhumuni ya ziara ya madaktari
na washauri hawa kutoka Hospitali za Apollo nchini Tanzania ni
kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata vipimo sahihi kwa gharama nafuu.
Madaktari bingwa watatu wanao ongoza katika Hospitali za Apollo
watafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Hindu
Mandal kutoa huduma za kimataifa kwa watanzania.
Wagonjwa
wanaougua magonjwa yanayohusiana na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu,
figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo, wanashauriwa kuhudhuria na
kushiriki tukio hili la kipekee. Madaktari watatembelea wagonjwa,
kufuatilia historia za wagonjwa na kuwashauri matibabu sahihi kutokana
na ripoti za matibabu na vipimo.
Daktari wa
kwanza atakayeshiriki katika kutoa ushauri na matibabu ni Dkt. Alok
Ranjan ambaye ni mtaalamu katika upasuaji mishipa ya fahamu na uti wa
mgongo katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad. Atapatikana siku ya
Jumatatu ya tarehe 27 Julai na tarehe 28 Julai kati ya saa 03 asubuhi
na 11 jioni kwa tarehe hizo mbili katika Hospitali ya Hindu Mandal
jijini Dar es salaam. Dkt. Alon Ranjan ni mtaalamu anayeongoza katika
upausaji wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kwa zaidi ya miaka 20 kwa
kufanya upasuaji mgumu wa mishipa. Dkt. Alok Ranjan ameongoza timu yake
kufanya pasuaji mbali mbali za mishipa ya fahamu zaidi ya 1,000 kama
vile upasuaji mdogo wa mtindio wa ubongo, upasuaji wenye madhara madogo
wa uti wa mgongo, upasuaji mgumu wa uti wa mgongo, na upasuaji kwa
kutumia kifaa maalumu cha kuangalia uti wa mgongo na ubongo.
Kliniki ya
ushauri na tiba ya pili imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 31
Julai na 01 Agosti katika Hospitali ya Hindu Mandal ya Dar es salaam.
Wagonjwa watapata fursa ya kupata ushauri na tiba kutoka kwa Dkt.
Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi na Dkt.
Sanjay Maitra ambaye ni mtaalamu wa figo kati ya saa 3 asubuhi na saa 11
Jioni kwa siku za Ijumaa na Jumamosi. Huduma hizi za ushauri na tiba,
zitatolewa kwa gharama nafuu.
Dkt.
Rajagopal amebobea katika magonjwa ya mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi
kwa wanaume. Amekuwa mshauri mwandamizi wa tiba wa magonjwa ya vina vya
uzazi katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad tangu mwaka 1994.
Dkt Sanjay
Maitra amebobea katika huduma na tiba za magonjwa ya figo na magonjwa
yanayo shabihiana na haya. Kwa kawaida madaktari hawa hutibu magonjwa
sugu ya figo, uvimbe katika figo, figo zilizoshindwa kufanya kazi na
jiwe figo ikiwa ni pamoja na kuelimisha juu ya masuala mbali mbali ya
upandikizaji wa figo na usafishaji. Dkt. Sanjay Maitra ana uzoefu wa
miaka mingi katika tiba ya figo na alimaliza masomo yake ya utaalamu wa
magonjwa ya figo kutoka katika chuo cha AIIMS mjini New Delhi. Dkt
Sanjay Maitra pia amekuwa akitoa mafunzo ya upandikizaji wa figo kutoka
katika miili iliyo kufa na iliyo hai, huduma muhimu za ubadilishaji wa
figo, usimamizi wa mda mrefu wa usafishaji wa figo kwa wagonjwa.
Hii siyo
mara ya kwanza kwa madaktari hawa kutembelea Dar es salaam. Ushirikiano
huu endelevu na Hospitali ya Hindu Mandal unathibitisha dhamira ya
Hospitali za Apollo katika kutoa huduma bora za afya na nia thabiti ya
kuendeleza mahusiano na Tanzania ambayo yameazishwa kwa Zaidi ya muongo
mmoja.
Katika siku
hizi ambazo madaktari hawa watatoa tiba na ushauri, Dkt. Alok Ranjan,
Dkt. Sanjay Maitra na Dkt. Rajagopal watakuwa wanapitia kujua hali za
wagonjwa ambao waliwahi kutibiwa mjini Hyderabad au ambao walitibiwa
kipindi ambacho madaktari hawa walitembelea Dar es salaam mara ya
mwisho. Katika kipindi hiki, madaktari hawa watafanya mahojiano na
wagonjwa kujua historia ya ugonjwa wao, kuwafanyia vipimo, kujadili
sababu zinazoweza kuwa vyanzo vya ugonjwa wao, matibabu yanayoweza
kutolewa inchini, kuwaandikia wagonjwa dawa na kufanya mipango ya vipimo
au kupendekeza matibabu ya ziada. Kwa baadhi ya wagonjwa, kutegemeana
na ukubwa wa tatizo la mgonjwa na hali yake, wagonjwa wanaweza
kushauriwa kutafuta matibabu zaidi nje ya nchi kwa matibabu ambayo
hayawezi kufanyika nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, wagonjwa
watajadiliana na madaktari majibu ya vipimo au ripoti za vipimo
vilivyofanyika hivi karibuni. Kliniki hii ni fursa ya kipekee kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yahusianayo na uti wa mgongo,
mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo na ambao
wanahitaji ushauri mbadala au wale ambao hawawezi kumudu gharama za
kupata matibabu nje ya nchi.
Ndugu
Radhey Mohan, Makamu wa Raisi wa Maendeleo ya Kimataifa Kibiashara
anadhamini kliniki hizi kwa kushirikiana na Hospitali ya Hindu Mandal.
Wagonjwa
wanahamasishwa kufaidika na kufursa hii na wanashauriwa kujiandikisha
kupata ahadi ya kuwaona madaktari hawa katika Hospitali ya Hindu Mandal
kwa kupiga simu nambari +255 22 211 4991-4
