kukoma kwa mapigano Ukraine bado Ndoto
Makubaliano ya kuacha mapigano mashariki ya Ukraine yaligonga Mwamba Viongozi wa Urusi, Ukraine,Ujer...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/03/kukoma-kwa-mapigano-ukraine-bado-ndoto.html

Viongozi
wa Urusi, Ukraine,Ujerumani na Ufaransa wamefanya mazungumzo zaidi kwa
njia ya simu kuhusu jitihada za kuhakikisha mapigani yanakoma Mashariki
mwa Ukraine.
Wamekubaliana kupeleka waangalizi katika maeneo kumi ambako makubaliano ya kusitisha mapigano yalikiukwa ukiwemo Mji wa Shchastya,Volnovakha na maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Donetsk.
Viongozi hao wamesisitiza kuhusu uhitaji wa kuwaruhusu waangalizi kufuatilia na kuhakikisha uondolewaji wa Silaha.
Petro Poroshenko, Angela Merkel na Francois Hollande kadhalika wamemtaka Rais wa Urusi Vladmir Putin kumuachia huru Nadya Savchenko, Rubani wa Ndege wa Ukraine aliyeshikiliwa tangu mwaka jana, amekuwa katika mgomo wa kutokula kwa siku 80.