UBUYU: Lulu na Jacqueline Wolper Waoneshana Jeuri ya Mabwana!
Warembo na waigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshan...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/02/ubuyu-lulu-na-jacqueline-wolper.html
Warembo na waigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Ijumaa, wamebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine.
Inadaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo.
Kwa mujibu wa vyanzo vyao ambavyo ni watu wa karibu wa mastaa hao, kwa sasa wawili hao ni moto wa kuotea mbali kwani kila mmoja amepata bwana mwenye ‘mpunga’ mrefu.
Inadaiwa kwamba, kama ilivyokuwa kwa Lulu, Wolper naye analipiwa nyumba hiyo kiasi cha dola za Kimarekani 1,500 kwa mwezi (zaidi ya Sh. milioni 2.4) karibia Sh. milioni 30 kwa mwaka.
Uchunguzi huo umeonyesha kuwa Lulu ana mkoko aina ya Toyota Rav4 New Model wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.Kwa upande wake Wolper anasukuma ndinga aina ya Toyota Prado, nalo lina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.
Ila jamani hawa si mastaa wakubwa na wanafanya kazi zakutosha kwanini tusiamini kuwa hivi kama kweli wanavyo ni matunda ya jasho lao!!
Picha juu ni nyumba zao zinadaiwa walizopangishiwa
