WHO:Laonya kusambaa kwa Ebola Mali
Margeret Chan wa WHO aonya kuhusu kusamabaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini Mali...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/wholaonya-kusambaa-kwa-ebola-mali.html

Mkuu wa shirika la afya duniani WHO Margaret Chan ameonya kuhusu kusambaa kwa ugonjwa wa ebola nchini Mali.
Ameuambia mkutano na waandishi habari mjini Washington kuwa watu 500 ambao walikaribiana na mhubiri mmoja wa kiislamu wako chini ya uchunguzi.Kundi la watu ambao walikuwa wamekaribiana na msichana aliyekuwa na ugonjwa wa Ebola wamekamilisa kipindi chao cha uchunguzi na sasa wameripotiwa kuwa na afya nzuri.
Naye katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliuambia mkutano huo wa wanahabari kuwa kuna matumaini kadhaa yakiwemo ya jamii zilizoathirika kubadili mienendo yao na pia uwezo wa kuwatibu wagonjwa.
Hata hivyo amesema kuwa ulimwengu ni lazima uendelee na jitihada zao ili kuzuia ugonjwa huo kuenea.