WATU KADHAA WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI WILAYANI KAHAMA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/watu-kadhaa-wafariki-katika-ajali-ya.html
Muonekano wa hali halisi katika eneo latukio
WATU
kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye
ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar
lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.
Chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa
kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni
na kupinduka.
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi
ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao
wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.
Taarifa zaidi pamoja na picha za ajali hiyo zitawajia hivi punde.
