WAJUE MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI.
BAADA ya wiki iliyopita kuwaletea marais wa Afrika waliofia madarakani. Yaani walikuwa wakiongoza nchi zao wakakumbwa na mauti. Wik...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/wajue-marais-waliouawa-kwa-kupigwa.html

BAADA
ya wiki iliyopita kuwaletea marais wa Afrika waliofia madarakani. Yaani
walikuwa wakiongoza nchi zao wakakumbwa na mauti. Wiki hii tunawaletea
marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani.
ABRAHAM
Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini
Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa
amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.
INDIRA Priyadarshini
Gandhi; alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na
walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.
JOHN Francis Kennedy
‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa
kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.
LAURENT Desire Kabila;
alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu
wanaosadikiwa ni walinzi wake.
THOMAS Isdor Noel
Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi
1984 alipouawa kwa kupigwa risasi na Blaise Compaore ambaye hivi
karibuni ameikimbia nchi hiyo.
WILLIAM Richard Tolbert
Jr; alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa
Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.
MUHAMMAR Muhamad Abu
Migar al Ghaddaf; alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa
kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya,
Oktoba 20, 2011.
ABEID Amani Karume;
alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa
kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi
kupatikana.
Jean baptist ouedraogo;
aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa
risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi
hiyo kabla na yeye kupinduliwa.