VIDEO DIAMOND AFUNGUKA MENGI KUHUSU WEMA ZARI NA WENGINEO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/video-diamond-afunguka-mengi-kuhusu.html

Tumekaa na Diamond Platnumz kuzunguma mambo kibao hususan tetesi
zinazoendelea sasa kuwa ameachana na mpenzi wake Wema Sepetu na kuwa ana
uhusiano na mfanyabiashara mrembo wa Uganda, Zari the Bosslady pamoja
na issue zingine. Itazame hapo chini au soma kwa kifupi baadhi ya kile
Kuhusu kwanini anatumia wazungu zaidi kwenye video zake Mimi nafikiri ni
kutokuwa na uelewa tu kwasababu inategema na concept. Ukiangalia kama
‘Mdogo Mdogo’ ilikuwa inazungumzia mapenzi hayaulizi kwanini so ilikuwa
lazima ioneshe pande mbili, kuna wazungu na mimi ni mwaafrika na familia
yangu ya kiafrika. Kuna mtoto wa kizungu ambaye ananizimia mimi
mwaafrika lakini familia yake haipendi ukizingatia wao ni wafalme na
nini. Lakini mtoto bado ananipenda hivyo hivyo, ananifuata mpaka porini
ananikuta kwenye maji naimba mimi kule. Mpaka dakika ya mwisho anakuja
baba yake anamkuta yupo kwetu kijijini anacheza na familia yetu sisi so
dakika ya mwisho unakuta mzee mwenye anakubali mwanae aolewe.
Sasa
huwezi kufanya familia ya kiafrika na familia ya kiafrika, haiwezi
kuleta maana, lazima iwe tofauti. Ukiangalia kama video ya ‘Ntampata
Wapi’ watu wanashindwa kuelewa, yule model sio mzungu. Ni mwaafrika
sababu anaishi south kaiva sana. Ukiangalia kuna waafrika, kuna
wazungu.. unajua ukiwachanganya inakufanya uweze kuwavuta na watu
wengine waconcentrate na ile nyimbo, waone kama hata sisi inatuhusu,
usifanye issue za kibaguzi.
Kuhusu anavyomchukulia model wa kwenye video ya Ntampata Wapi, Melissa

Kiukweli amejitahidi na amefanya vizuri sana. Bado tunawasiliana,
hata juzi nilimtumia meseji nikamwambia ‘Melissa natamani ujue jinsi
gani unazungumziwa, nikasema ‘najua kabisa huko South Africa hawawezi
kuwa wanaizungumzia hii video kama wanavyoizungumzia hii video huku
nyumbani, natamani ujue jinsi gani walivyokupokea, natamani ujue
umefahamika kiasi gani.
Nikamwambia ‘siku ntakutag Instagram, halafu utaona shughuli yake.’
Ntamuweka siku moja Instagram, najua watu wanasubiri akaunti yake.
Kuhusu kufanya kazi na Yemi Alade kwenye kipindi cha Coke Studio Africa
Kiukweli mimi nafikiri ilikuwa ni kama zari. Kitu ninachompendea Yemi
Alade kwanza yeye mwenyewe ni mtu mwendawazimu fulani akifika kwenye
stage, ni chizi muziki, akifika kwenye muziki anakuwa hana haya. Unaweza
ukatoa pande la haraka haraka ‘mwanangu tugonge hivi, akagonga’ ni mtu
wa miongezeko na yuko charming.
Kuhusu remix ya wimbo ‘Kissing’ wa Yemi ambao Diamond alishirikishwa
Kuna vitu fulani ilitakiwa virekebishwe kwasababu Yemi aliniambia
atakuja Tanzania kwasababu tufanye video ya ile remix , kuna njonjo
fulani zinatakiwa ziongezeke, so alikuwa na plan ya kushoot video ya
remix, nikamwambia ‘that’s a good idea.
Kuhusu tetesi kuwa ameachana na Wema Sepetu
Unajua mahusiano ya umaarufu yana mazuri na madhara yake, so lazima
uwe na akili ya ziada kuweza kujua unazungumza vipi kuhusu masuala yenu
na unaweza vipi kuhandle mambo yenu, either kwenye mambo mazuri au
mabaya.
Ndio maana kuna vitu vingine vinafaa kuwa vinatoka, vingine vinakuwa
havifai. So situation iliyopo kuanza kuisema katika media ikiwa haikuwa
tayari inakuwa sio vizuri kwasababu mtu anaweza akakutafsiri vibaya
mwingine akakuona kama unaongea sana, hauna roho ya kiume.
So kuna vitu fulani ambavyo lazima viwe na muda muafaka kwamba najua
huumuda sasa hivi vinaweza kuweka hadharani na watu wakasikia, najua
watu wanataka kusikia, watu wanatamani kusikia kauli kutoka pande zote.
Kuhusu picha ambayo yeye na Zari the Bosslady wanaonekana wakipigana busu
Unajua kwenye movie kuna watu wanakuwa kabisa kama wanakulana, hawana
nguo kabisa so ukiangalia kwa mtazamo mfupi unaweza ukaona kabisa hawa
walikuwa wanamegana, that’s what we said before, it’s a project, project
inabeba vitu vingi ndani yake. Unajua ilikuwa rahisi kutoka mwanzo
kuzungumza kwamba project yenyewe ni hii na hii, lakini sasa ukisema
unakuwa unaua kick ya project. Lazima watu waisubiri kwa hamu, kwa
heshima na taadhima kama inadondoka lini, ila nafikiri muda wake umebaki
mchache sana.
Kuhusu Wema Sepetu na Penny kupatana
Mimi nafikiri ni kitu kizuri. Wanapokuwa wanapatana kwanza inakuwa ni
heri inatengeneza njia na mifano bora hata kwa wanawake wengine kufuta
zile zama za kijinga na maneno ambayo yalikuwa yakiandikwa. Kwahiyo mimi
nafurahi, halafu ukizingatia mimi ni muislamu naweza nikaoa wanawake
wanne.Kuhusu kama yeye na Penny hawapatani tena
Kiukweli sijawahi kupotezeana na Penny kabisa, ni mwanangu sana,
nisiwe mnafiki. Hata hapa katikati alikuwa akinipa deal nyingi sana za
kazi na nini. Ni mwanangu yaani, mimi namuitaga ‘Aunt Penny’, na yeye
ananiitaga ‘Uncle Chibu.’
Kuhusu taarifa kuwa Jose Chameleone alimuomba collabo
Kwanza nilipoona kimeandikwa, kilinisikitisha, lakini kwasababu
naiheshimu Bongo5 sikuweza kuikanusha. Ni story ambazo si za ukweli.
Mimi na Chameleone ni mtu ambaye huwa tunazungumza vitu vya kimaendeleo.
Nakumbuka mawasiliano yangu na Jose nilimwambia ‘Jose mimi nakuheshimu
sana kwasababu aliniambia ‘unafanya vizuri sana mdogo wangu’ nikamwambia
‘nashukuru lakini jua nakuheshimu sana, kwasababu mimi nimeanza
kukusikia sijui nitatoka lini.
Mpaka leo mimi ninatoka, nakukuta bado unafanya vizuri’. Nikamwambia
‘Bro hongera sana mimi nimeshaona watu wengi sana wanakuja, wanatoka
wanaondoka’. Yaani nilimwambia ‘kaa ukijua mimi nakuheshimu sana,’ so
huwa nachat naye vizuri tu.
Ilivyotokea ile issue, nakibaki ‘sijui nafanya vipi’ Nikasema
nikianza kumtext Jose, atanihisi kama najishtukia, ikabidi nikae kimya.
Juzi kati akanitafuta Profesa, akaniambia ‘nina ujumbe wako kutoka kwa
Jose, akaniambia ujumbe wako ‘ni hivi na hivi’.
Sasa mimi nikamwambia ‘bro, mimi kinachonisikitisha Jose ni mtu
ambaye mimi ninaongea naye, tena nikiongea naye naongea kwa heshima na
taadhima, ameshindwa vipi kunitext au kunuambia, mdogo wangu hili suala
likoje? Kwanini hajaniambia! Nina kila sababu ya kumheshimu Jose, kwanza
kanizidi umri, kanizidi kimaendeleo, kwahiyo kikitokea kitu halafu
akikichukulia moyoni, bila kuniambia naona haiwezi kwenda hivyo.
Kuna kampuni inaitwa Mziiki ambayo mimi ni balozi na Jose pia ni
balozi wa Mziiki ambapo inakiwa tufanye wimbo wa Mziiki lakini hatujakaa
kuzungumza labda Jose kuniambia ‘nataka tufanye collabo. Hata
tukizungumza masuala ya kufanya nyimbo, hatuzungumzii kwamba kuna mtu
kwamba anataka msaada au anataka booster, kiukweli hizi habari
zimenisikitisha sana. Na mimi sio kwa kufikiria tu, nina imani lazima
kutakuwa na watu wananichonganisha sana na Jose.
Kwa sababu kuna kipindi katikati aliniblock kwenye Instagram.
Nikamwambia ‘mbona sikupati bro’ kwasababu najua kuna watu wengi
wanaweza kumpelekea mambo mabaya mabaya ya kutaka anichukie mimi. Lakini
kiukweli mimi sijazungumza kauli hizo, hata kama Jose atakuwa
anatazama, ajue hivi ni vitu vya uongo na vitu ambavyo vinatungiwa.
BOFYA HAPA
BOFYA HAPA