TAARIFA NYINGINE KUHUSIANA NA MZIGO MKUBWA WA DAWA ZA KULEVYA.
Bado taarifa za watu kukamatwa na dawa za kulevya zimeendelea kuchukua nafasi, ni siku chache zimepita tangu Polisi wa Nigeria kum...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/taarifa-nyingine-kuhusiana-na-mzigo.html

Bado
taarifa za watu kukamatwa na dawa za kulevya zimeendelea kuchukua
nafasi, ni siku chache zimepita tangu Polisi wa Nigeria kumkamata mtu
ambaye alikuwa anasafirisha dawa za kulevya akiwa amefisha ndani ya
viatu vya kike ndani ya mabegi makubwa mawili, leo kuna watu wengine
wane wamekamatwa wakisafirisha mzigo wa dawa hizo.
Polisi wa Mombasa, Kenya wamesema wanawashikilia watu wanne kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine.

Askari Polisi wa Kenya.
Mpelelezi
ambaye anafanya kazi na kikosi cha kuzuia Mihadarati, Kenya
Anti-narcotics Unit, Hamis Masha amesema watu hao wanadaiwa kuhusika na
mifuko 98 za dawa hizo zilizokamatwa Nairobi na walikuwa wakitafutwa na
maafisa wa usalama wa Marekani wa DEA.
Maafisa
hao wamesema dawa hizo huwa zinasafirishwa kutoka Pakistan na Iran na
kuingia katika bandari za Afrika Mashariki ambako kuna ukaguzi duni wa
bidhaa zinazoingizwa na baadaye kupelekwa Ulaya.
Watu hao waliokamatwa wawili wana asili ya Kenya na wawili asili ya India.