PICHA: YALIYOJIRI JANA BUNGENI MJINI DODOMA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/picha-yaliyojiri-jana-bungeni-mjini.html
Spika wa
Bunge Mhe. Anna Makinda akiliongoza Bunge mjini Dodoma jana,wakati
akitoa ufafanuzi kuhusu mtu mmoja kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma kwa kosa la kupatikana akisambaza Ripoti ya (ESCROW) ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Sheria Baada ya Hoja
iliyoibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia.

Mbunge
wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia akiwa amekaa na Hasimu wake wa Siasa jimbo
la Vunjo Mhe.Agustino Mrema wakimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge
Mhe.Anna Makinda.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana ya wanachama wa chama cha kuweka na
kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda. Aliye valia gauni la njano ni
Mbunge wa Busanda Mhe.Lolesia Bukwimba.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda.

Mbunge wa
Busanda Mhe. Lolesia Bukwimba (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya juu ya ugeni wake wa
wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka
Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka
Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma.

Waziri wa
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sofia Simba (kushoto)
akifurahia jambo na Mhe.Anna Mkinda wakati wakitoka katika kikao cha
Bunge. Picha zote na Deusdedit Moshi
