NAJIVUNIA KUZAA NA MKE WANGU SIWEMA 'NAY WA MITEGO'
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa japokuwa ana watoto wengine wa nje lakini anajivuni...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/najivunia-kuzaa-na-mke-wangu-siwema-nay.html
MWANAMUZIKI
wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa
japokuwa ana watoto wengine wa nje lakini anajivunia kuzaa na mkewe,
Siwema kwani walipitia changamoto nyingi kabla ya kupata mtoto.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.
Akichezesha
taya na paparazi wetu, Nay alisema katika maisha ya mapenzi yake na
Siwema walivumilia vingi na hivi sasa ana mshukuru Mungu kwani wameweza
kufikia hatua nzuri ya kupata mtoto.
“Maisha ya mapenzi yetu
yalikuwa na changamoto sana lakini nilisimama kwa sababu nampenda mke
wangu Siwema, najivunia kuzaa na Siwema mtoto wa kiume na ninaendelea
kumuomba Mungu aendelee kumkuza mwanetu,” alisema Nay wa Mitego.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego
Wadau
mbalimbali wamekuwa wakimpongeza Nay kwenye mitandao ya kijamii kwa
kile wanachodai kwamba ana mapenzi ya kweli licha ya changamoto nyingi
zilizojitokeza kwa mpenzi wake Siwema za picha kuzagaa mitandaoni kwamba
alikuwa mchumba wa mtu.