MWANAMKE AHIFADHIWA MASAA 11 MONCHWARI AKIDHANIWA AMEKUFA
Story za maajabu ya ulimwengu zinaendelea kukaa kwenye headlines kila siku, na inaponifikia cha kwanza ninachokifanya ni kukufikis...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mwanamke-ahifadhiwa-masaa-11-monchwari.html
Story
za maajabu ya ulimwengu zinaendelea kukaa kwenye headlines kila siku,
na inaponifikia cha kwanza ninachokifanya ni kukufikishia mapema
iwezekanavyo ili na wewe usipitwe.
Ya
leo inaweza kuwa moja kati ya zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu
mwanamke Janina Kolkiewicz raia wa Poland, mwenye umri wa miaka 91
ambaye amekaa kwa muda saa 11 katika chumba cha kuhifadhia maiti huku
mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada ya kuthibitishwa na daktari wa
familia yake kwamba amefariki, muda mfupi baadaye wahudumu wa mochwari
waligundua kwamba ni mzima baada ya kuhisi anatikisika ndani ya mfuko
alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea mochwari, alilalamika kuhisi baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya moto na mkate.
Daktari
aliyethibitisha mauti ya mtu huyo anasema hata yeye anashangazwa na
tukio hilo kwani vipimo vyote vilionyesha kuwa mapigo ya moyo yalisimama
na hakuwa hai.
Taarifa
za kuwa hai mwanamke huyo zilimshtua kila mtu kwenye familia yake na
kujikuta ikibatilisha hati ya kifo iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake
ambayo yalipangwa kufanyika siku mbili baadaye.
