MREMBO WA HONDURAS ALIYEKUWA ASHIRIKI MISS WORLD KESHO AUAWA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mrembo-wa-honduras-aliyekuwa-ashiriki.html
Mrembo wa Honduras amekutwa amekufa siku chache kabla ya kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) yaliyopangwa kufanyika jijini London, Uingeraza, Polisi imesema.
(Reuters)
Mtandao wa Reuters umeripoti muda mfupi uliopita kuwa miili ya Maria Jose Alvarado (19), na dada yake Sofia ilikutwa imezikwa karibu na mto katika mkoa wenye milima wa Santa Barbara, km 180 (mail 110) kutoka mji mkuu Tegucigalpa, alisema Leandro Osorio, mkuu wa idara ya upepelezi.
Alvarado alikuwa akijiandaa kwa shindano la urembo wa dunia lililopangwa kufanyika kuanzia leo na kufikia tamati Desemba 4, mwaka huu jijini London.
Yeye na dada yake walipotea tangu Alhamisi ya wiki iliyopita wakati walipoonekana wakiondoka kwenye sherehe wakiwa kwenye gari ambalo halikuwa na namba za usajiri wa gari.
“Ninathibitisha kwamba madada Alvarado wameonekana… Tumepata pia silaha iliyotumika kuua na chombo cha usafiri kilichotumika kuwasafirisha hadi sehemu waliyozikwa,” Osorio ameviambia vyombo vya habari nchini Honduras.
Waziri wa Mambo ya Ndani Arturo Corrales ameviambia vyombo vya habari vya Honduras kwamba Plutarco Ruiz, ambaye ni mchumba wake na dada wa malkia huyo, ndiye aliyehusika na mauaji.
Honduras ni nchi moja ya nchi zinazoongoza kwa mauaji ya watu ulimwenguni, takwimu zikionesha kwamba kati ya watu 100,000, watu 90 huawa ikiwa ni karibu mara mbili ilivyo katika nchi za Venezuela, Belize na El Salvador.
Meximo ndiyo nchi inakamata nafasi ya kwanza kwa mauaji ya watu duniani, huku asilimia kubwa ya mauaji yakisababishwa na dawa za kulevya.