Mkutano wa OPEC Vienna
Wanachama wa nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani wa shirika la OPEC wanakutana katika mkutano mgumu kabisa hasa kutokana na ha...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mkutano-wa-opec-vienna.html
Wanachama wa nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani wa shirika la
OPEC wanakutana katika mkutano mgumu kabisa hasa kutokana na hatua ya
kushuka kwa bei za mafuta kwa asilimia 30 tangu Juni.
Nchi 12 wanachama wa shirika la Opec wanakutana baadae mjini Vienna
nchini Uswisi katika mkutano unaotajwa kuwa mgumu na muhimu zaidi huku
wanachama hao wakitolewa mwito wa kuchukua hatua za kueleweka baada ya
bei za mafuta kushuka kwa asilimia 30 tangu mwezi Juni.Mataifa ya Ghuba yanayotoa mafuta kwa wingi yakiongozwa na Saudi Arabia yanatarajiwa kuzihimiza nchi nyingine wanachama kutochukua hatua ya kupunguza uzalishaji licha ya baadhi ya wanachama kusikika wakitoa miito ya kupunguza uzalishaji wa mafuta ghafi kama hatua ya kuimarisha bei za bidhaa hiyo muhimu duniani iliyokwisha teremka vibaya.
Bomba la Mafuta NigeriaWanachama wengine kama Venezuela au Iran zitakabiliwa na hali ngumu zaidi ikiwa hilo litafanyika.Waziri wa mafuta wa Iran Bijan Zangeneh akizungumzia suala hilo amesema baadhi ya wanachama wa Opec wanaamini kwamba huu ndio wakati wanaohitajika kutetea masoko yao.wakati wataalamu katika soko la bidhaa hiyo wakiamini kwamba kwa sasa kiwango kilichoko kimepindukia na mwakani kitapindukia zaidi.
Kiwanda cha mafuta cha kampuni ya Shell Carlifonia MarekaniIkiwa upande mmoja utachukua uamuzi wa kupunguza kiwango cha uzalishaji wa mafuta basi hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwa shirika hilo la OPEC linalotegemewa kwa thuluthi tatu ya mafuta ya dunia. Lakini hatua hiyo itakuwa pigo kwa soko la mafuta ghafi yanayozalishwa na nchi za Amerika ya Kaskazini. Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi lakini wanahisi mkutano wa Vienna unaofuatiliwa kwa karibu utaamua kubakia na uzalishaji wa mapipa millioni 30 kwa siku kama ilivyo sasa ingawa vile vile upo uwezekano wa kufikia hatua tofauti na hiyo.
Mwandishi Saumu Mwasimba
