MH, RAISI KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA AMIGOLAS WA TWANGA PEPETA
Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/mh-raisi-kikwete-atuma-salamu-za.html

Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Profesa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Mwanamuziki Muasisi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta, na baadaye Kiongozi wa Bendi ya Ruvu Star, Khamisi Kayumbu maarufu kama Amigolas (pichani).
“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mwanamuziki Khamisi Kayumbu kilichotokea tarehe 9 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amesema anatambua mchango mkubwa wa Marehemu Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu, kupitia sanaa ya muziki katika kuwafikishia…

Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Profesa Jakaya
Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi kwa Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara
kuomboleza kifo cha Mwanamuziki Muasisi wa Bendi Maarufu ya Twanga
Pepeta, na baadaye Kiongozi wa Bendi ya Ruvu Star, Khamisi Kayumbu
maarufu kama Amigolas (pichani).“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mwanamuziki Khamisi Kayumbu kilichotokea tarehe 9 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amesema anatambua mchango mkubwa wa Marehemu Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu, kupitia sanaa ya muziki katika kuwafikishia wananchi ujumbe muhimu wa masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa Hayati Kayumbu alikuwa mfano unaofaa kuigwa na Wasanii wengine kote nchini.
“Kutokana na msiba huu, naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa Wanamuziki Mahiri hapa nchini, na Rambirambi hizi ziwafikie pia Wanamuziki
wengine kote nchini kwa kumpoteza mwenzao”.
Aidha, Rais Kikwete amemwomba Dkt. Fenella Mukangara kumfikishia Salamu zake za Pole kwa Familia ya Marehemu Khamisi Kayumbu kwa kupotelewa na Kiongozi na Mhimili
madhubuti wa Familia.
Mwisho.
Imetolewa
na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Novemba,2014