MAKAVU LIVE! MASTAA WA KIKE BONGO MOVIES MTAIGIZA MAISHA YENU HADI LINI?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/makavu-live-mastaa-wa-kike-bongo-movies.html
Mastaa
wa Bongo Movies. Bila shaka mko poa na mnaendelea na harakati zenu za
kila siku, najua mna mishemishe nyingi kweli japo najua nyingi ni za
starehe zaidi.Binafsi mimi niko poa naendelea na majukumu yangu ya kila
siku ikiwemo hili la kuwaandikia barua. Madhumuni ya barua hii ni kama
inavyojieleza hapo juu katika kichwa chake cha habari.
Ndugu
zangu, nimekuwa nikifuatilia aina ya maisha mnayoishi kwa muda mrefu
nimegundua wengi wenu mnaishi maisha ya kuigiza kama vile mnavyofanya
kwenye filamu zenu. Hamtegemei kazi zenu kuendesha maisha bali mnatumia
‘njia’ mbadala ili kulinda heshima ya umaarufu wenu, siyo sawa.
Mnataka
kuonekana mnakula katika mahoteli ya gharama, nyumba za gharama,
kubadili mavazi kila siku, kuendesha magari ya kifahari na kila aina ya
starehe mjini ili muweze kwenda sawa na wenye nazo.Ufahari mnaouonesha
haufanani kabisa na pato mnaloingiza kwenye filamu (mifano ipo mingi
tu).
Natambua
kabisa bei ya sinema moja mnavyoiuza kwa wahindi au kwingineko,
haitoshi kabisa kufanya vurugu ambazo mnazifanya kila siku wakati wengi
wenu hata hamzalishi hata muvi tatu kwa mwaka.Dada zangu nataka tu
niwakumbushe kwamba maisha si starehe tu, maisha yana maana kubwa kama
mtajiheshimu na kutengeneza mazingira mazuri ya kutegemea kipato cha
sanaa yenu, kuiboresha kwa kuwekeza nguvu na akili nyingi.

Sitaki kuwataja kwa
majina kwa leo lakini naamini mnajijua. Kwa nini msifanye kazi kama
baadhi ya mastaa wa kiume ambao tunawaona wanaingiza fedha na kuendesha
maisha yao kupitia filamu wanazozizalisha? Kwa nini msiige mifano kutoka
kwa dada zetu wa Nigeria ambao wanategemea sanaa kutengeneza mamilioni?
Badala
msimame katika mfumo mzuri wa kuzalisha sinema kwa nguvu na akili zenu
zote, nyinyi mnatumia njia ya mkato kujiingizia fedha. Madhara yake
ndiyo mnajikuta mkiingia katika mtego wa kujiuza kama ilivyotokea kwa
Jack Pentezel ‘Jack wa Chuz’, Aunty Lulu na Baby Madaha.
Ni
rahisi mtu kuwarubuni kwa fedha, kuwanunulia magari ya kifahari na
nyinyi mkaridhika na kuona mmeyapatia maisha. Kesho na kesho kutwa ndiyo
haohao wanaokuja kuwanyang’anya baada ya kuwatumia vya kutosha sababu
wanakuwa hawajawakabidhi kadi.
Ni
aibu hata kwa mashabiki wenu ambao wanawafuatilia kupitia filamu.
Wanavyoona mnaigiza maisha katika mitandao ya kijamii wanapata hamasa
kwamba sanaa inawalipa kumbe kiuhalisia haiwalipi.Jamani badilikeni kwa
kujituma katika kuigiza ili heshima ya majina yenu itokane na sanaa.
Naamini
inawezekana kwani vipaji mnavyo na hakuna ubishi mnaweza kuibadilisha
tasnia kama wenyewe mtaamua kufanya hivyo. Kwa leo acha niishie hapo,
badilikeni!
Wasalaam
Erick Evarist

