KIBAKA ANUSURIKA KUFA KWA KUPORA SIMU DUKANI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/kibaka-anusurika-kufa-kwa-kupora-simu.html

Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa kile walichomtuhumu kuiba simu katika moja ya duka lililopoa maeneo ya Makumbusho karibu na Kituo cha Daladala, jijini Dar es Salaam.
Wakielezea
tukio hilo mashuhuda walisema kuwa kijana huyo aliingia katika duka
hilo lililokuwa na mwanadada na kupora simu iliyokuwa juu ya kabati la
bidhaa na kutimka nayo jambo lililomfanya mwanadada huyo kutoka nje na
kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Kama
ilivyo kawaida kijana huyo aliungaishiwa na kila mtu aliyemuana akitimka
na kufanikiwa kumtia nguvuni na kuanza kula kichapo hadi aliporejesha
simu ya mdada huyo. Baadaye aliachiwa huru na kuondoka zake.
Kjana huyo akijibu maswali baada ya kichapo.
Kijana huyo akijificha chini ya ua akihisi kuwa hapo ni mahala salama kwa wakati huo baada ya kula kichapo....
Akipiga kelele na mayowe kuomba msamaha asiendelee kula kichapo.
Akimng'ang'ania kijana akiyemuokoa ili amsindikize kutoa eneo hilo lenye ngumi za moto kuliko maelezo...



