BABY MADAHA AFUNGUKA SITUMII KINGA 'KONDOM' HATA SIKU MOJA
BAADA ya hivi karibuni Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Baby Madaha kusema ameamua kuwapanga wanaume, hivi sasa ameibuka na jipya n...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/baby-madaha-afunguka-situmii-kinga.html
BAADA
ya hivi karibuni Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Baby Madaha kusema
ameamua kuwapanga wanaume, hivi sasa ameibuka na jipya na kudai kwamba
huwa hatumii kinga ‘kondom’ hata siku moja.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Baby Madaha alisema kabla hajaanguka penzini na
mwanaume lazima akapime kwanza Ukimwi na baada ya hapo ndipo mambo
mengine yanaendelea hivyo akishahakikisha huyo mwanaume ni mzima huwa
ahangaiki kutumia kinga.
“Japokuwa nawapanga
wanaume lakini najali sana afya yangu yaani kila baada ya miezi mitatu
huwa naenda kupima kabla sijaingia naye kwenye uhusiano, nikikuta yuko
fresh tunaendelea na mapenzi yetu na huwa situmii kinga kwa sababu
nakuwa nimeshajua afya yake.
Ikitokea amenizingua nampiga chini namchukua mwingine naenda kumpima hivyohivyo maisha yanasonga mbele,” alisema Baby Madaha.
