BAADA YA KUVUA TAJI LA MISS TANZANIA! SITTI MTEMVU AAMUA KUVUA TAJI LA MISS TEMEKE PIA
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu. HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/baada-ya-kuvua-taji-la-miss-tanzania.html
HAIJAKAA sawasawa!
Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss
Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri
wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine wakimtaka avue mataji
mengine mawili.
Baadhi
ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu
iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya
kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe
na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss
Tanzania na kushinda.
Wadau
hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia vitongojini,
wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo ya
kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana sifa
za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza
kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu ya
kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli
amedanganya, anajijua.
“Kama
angekuwa hajadanganya, kwa nini asitoe paspoti yake inayomwonesha ana
umri wa miaka 23? Mambo yalimfika shingoni ndiyo maana. Anachotakiwa ni
kuvua taji la Miss Chang’ombe na Miss Temeke mwaka huu,” alisema Ismail
Chandu, mkazi wa Temeke jijini Dar.
Shindano
la kumsaka Miss Chang’ombe lilifanyika Juni 27, mwaka huu kwenye Ukumbi
wa TCC Chang’ombe, Dar ambapo Sitti aliibuka kidedea akifuatiwa na
Paulina Elisante (anayetakiwa kuchukua taji), wa tatu ni Derena David.
Shindano
la Miss Temeke 2014 lilifanyika Agosti 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa
TCC Club, Chang’ombe jijini Dar ambapo Sitti Mtemvu aliibuka kidedea
akifuatiwa na Salama Saleh (anayetakiwa kushika nafasi ya kwanza) na
nafasi ya tatu ilitwaliwa na Neema Mollely.
Novemba
5, mwaka huu, Sitti Mtemvu aliiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania
inayoongozwa na Hashim Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake kuvua
taji hilo.Sitti alifikia uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo ya
kudanganya umri wakati akigombea taji hilo.
>>>>>GPL
