AUNT EZEKIEL, ODAMA WATIMULIWA BONGO MOVIE KISA KUWA KARIBU NA STEVE NYERERE
Mwanadada anaye tamba katika tasnia ya filamu bongo, Aunt Ezekiel
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/aunt-ezekiel-odama-watimuliwa-bongo.html
UPEPO mbaya
unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii
umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na
Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya
kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’.
Kwa
mujibu wa chanzo makini kilichozama katika kikao kilichofanyika
juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve
kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja
hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.
“Wamewaengua
baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni
mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye
msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika
majina ya wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.
Staa wa filamu bongo Devota Mbaga.
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama
hai lakini si wanachama wenye msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu
wa kuwa karibu na Steve Nyerere ambaye sasa anafanya harakati zake peke
yake.
Baada
ya habari hizo kutua katika rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea
hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:
Mkali wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka 'Odama'.
Devotha:
Mimi ndiyo kwanza nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata
habari za kikao hicho na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni
mwanachama hai na ni miongoni mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba,
lakini kama wameamua hivyo sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho
wa maisha.
Odama:
Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama,
watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote
ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.

