ASKARI POLISI 54 WAFUKUZWA KAZI KWA RUSHWA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/askari-polisi-54-wafukuzwa-kazi-kwa.html
Askari
54 wa jeshi la polisi nchini Tanzania wamefukuzwa kazi katika kipindi
cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu kutokana na kujihusisha na
vitendo vya rushwa.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Pereira Ame Silima amesema kuwa
kila mwaka serikali inapoteza wafanyakazi wengi kutokana na kujihususha
na vitendo vya rushwa.
Mh.
Silima ameongeza kuwa askari wengi wakishahitmu na kuingia kazini licha
ya viapo wanavyokula lakini wanageuka kuwa wahalifu hivyo jeshi la
Polisi nchini limewafukuza askari wote waliokutwa na Tuhuma za Rushwa.
