PICHA: HALIMA MDEE NA WANACHAMA WA CHADEMA WALIOANDAMANA KUELEKEA IKULU, WAKIONA CHA MOTO TOKA KWA POLISI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/picha-halima-mdee-na-wanachama-wa.html
Mwenyekiti wa BAWACHA
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa
katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea
ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya
iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali
walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na
kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja
na wafuasi wake na kupelekwa polisi Osterbay leo.
Polisi wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo
Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi

Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.

Halima mdee akizozana na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
Wafuasi wa chadema
wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay
wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa
mwenyekiti wao Halima Mndee
Wafuasi wa chadema wakilalamika kwa polisi
Kituo cha polisi cha Osterbay kilikuwa na ulinzi wa kutosha na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia kituoni hapo
Polisi wa Osterbay wakizuia gari kupitia
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay
Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay