NewsUpdates: Picha na Taarifa za awali kijana akutwa kafa katika korongo la Lubengela mkoani Kigoma
Mwili ukiwa bado eneo la tukio
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/newsupdates-picha-na-taarifa-za-awali.html
![]() |
| Mwili ukiwa bado eneo la tukio |
Katika
hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la
Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la
Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji
huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso,
Mara
baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na
kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo
haikujulikana maramoja imeandikwa nini
tukio hilo limetokea leo Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo,
katika
uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea jana usiku kwani
kutwa nzima ya jana hapakuonekana mtu ambae amekufa eneo,akiongea na
kibonajoro.com mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na
ambae ni mfanyakazi katika ofc moja jirani na eneo la tukio jina (....)
amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu
kukutwa ameuwawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo tunaviomba vyombo
vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili
linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.
Polisi wakichukua vielelezo katika picha
Kutokana
na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa
walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gali la
emegency la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari mwili
kupandishwa juu kupelekwa eneo husika,
Mwili ukitolewa tayari kupelekwa kwenye gari la Polisi
Mwili ukiingizwa kwenye gali la Polis kuelekea Central Polis kwa taratibu zingine
Mwili wa kijana Yusuph ukiwa ndani ya gari la Polisi,katika
taarifa zingine zilizopotikana eneo la tukio zinasema kabla ya
kugundulika kwa tukio hili kumetokea tukio lingine linalofanana na hili
maeneo ya mwasenga usiku wa kuamkia leo mtu kukutwa ametupwa huku akiwa
amepoteza maisha.
Polisi wakiondoka eneo la tukio
kwambali ndio eneo la ofisi za CCM mkoa ambapo kulia ndiko kumetokea tukio hili
















