NEWS ALERT: LORI LA MAFUTA LAWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/news-alert-lori-la-mafuta-lawaka-moto.html
Sehemu
ya Mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo
mara baada ya kupiga mweleka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari
lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani
bila ya tahadhari,hali iliyolipelekea Lori hilo kukosa mwelekeo na
kupiga mweleka.
Lori hilo pamoja na kupiga kwake mweleka
halikuwa na madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto.Baada ya
muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na
kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea
kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza lori hilo.
haijafahamika
mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliepoteza maisha katika moto huo,ila
hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na
eneo la tukio zimeteketea kwa moto,ambazo moja ni ya makazi ya watu,duka
la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni.
tutaendele kujuzana.
Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.

Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.
Picha na Eddymoblaze