NAY WA MITEGO KUINGIZA SOKONI MADAFTARI YAKE YA SHULE YATAITWA MR NAY
Rapper Nay wa Mitego amesema anatarajia kuzindua mradi wake wa madaftari ya shule kwaajili ya wanafunzi wa chekechea, shule ya msing...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/nay-wa-mitego-kuingiza-sokoni-madaftari.html
Rapper
Nay wa Mitego amesema anatarajia kuzindua mradi wake wa madaftari ya
shule kwaajili ya wanafunzi wa chekechea, shule ya msingi na sekondari
na vyuo vikuu.
Akiongea
na 255 kwenye kipindi cha XXL, Clouds FM, Nay amesema pamoja na kufanya
muziki yeye ni mfanyabiashara na anaamua kuwekeza ili hata kama muziki
ukigoma awe ni kitu cha kumuingizia kipato.
“Nimeamua
kutengeza madaftari yangu, kuna madaftari ya Mr Nay yatakuwa yanatoka.
Ni madaftari ya kawaida na counter books ambazo zitakuwa zikisambazwa
kuanzia nursery, primary, sekondari mpaka vyuo.
Nay amesema tayari ameshapata tenda ya kusambaza vifaa hivyo mkoani Mara. “Ni kitu ambacho tayari kiko confirmed,” amesisitiza.
Amesema madaftari hayo yataingia sokoni mwishoni mwa mwezi wa 12.