MENEJA WA ZAMANI WA REAL MADRID KUINOA GHANA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/meneja-wa-zamani-wa-real-madrid-kuinoa.html
Bernd
Schuster yupo katika orodha ya makocha watano ambao wanawania nafasi ya
ukocha wa timu ya taifa ya Ghana, hizi zikiwa ni taarifa za shirikisho
la soka nchini la nchi hiyo.
Bosi
huyo wa zamani wa Real Madrid hakufikiriwa kuipigania kazi hiyo kabla
ya kujitoa kwa Patrick Kluivert katika mchakato huo kiasi kupelekea
kuingia kwa mjerumani huyo katika orodha ya wapigania kazi hiyo.
Michel
Pont na Marco Tardelli watakutana na FA ya Ghana Oktoba 17, kabla ya
Avram Grant na Juan Ignacio Martinez kufuatia siku itakayofuata wakati
taifa hilo likiwa katika harakati za kusaka bosi mpya baada ya kuachana
na James Appiah kwa hiari yake mwezi Septemba.
Appiah
alikuwepo katika benchi katika kipindi cha miaka miwili na nusu na
kukiongoza kikosi hicho kikienda sare ya bao 1-1 na Uganda mchezo wa
kuwania kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika na baadaye wakipata ushindi
wa bao 3-2 dhidi ya Tog