MELI YA MAREKANI YAZUIWA KUTIA NANGA MEXICO KISA EBOLA
Meli ya Carnival Magic ya Marekani (Picha na Maktaba).
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/meli-ya-marekani-yazuiwa-kutia-nanga.html
Meli ya Carnival Magic ya Marekani imezuiwa kutia nanga katika kisiwa cha Mexico cha Cozumel ikihofiwa kuwa na mgonjwa wa Ebola.
Meli hiyo iliondoka katika jimbo la
Texas ikiwa na mhudumu mmoja wa afya ambaye alikuwa amehudumia sampuli
za mgonjwa wa ebola marehemu Thomas Duncan aliyeaga dunia kutokana na
ugonjwa huo.
Mhudumu
huyo wa afya ambaye amejitenga pamoja na mumewe wakiwa kwenye meli hiyo
yuko chini ya uangalizi kwa ameonyesha dalili za ugonjwa huo.

