KINACHOWAPONZA WEMA, KAJALA HIKI HAPA!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kinachowaponza-wema-kajala-hiki-hapa.html
KAMA walivyo
Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel kwa sasa ndivyo walivyokuwa Wema na
Kajala Masanja miezi kadhaa iliyopita.Wema na Kajala walikuwa mashosti
wa kufa mtu, walishibana na kupeana siri zao zote hususan zile za ndani
kabisa.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ .
Kudhihirisha
kwamba wameshibana, kuna wakati Wema aliamua kujitolea Sh. Mil 13
kulipa faini ambayo ilimnusuru Kajala kuswekwa gerezani.Baadaye walikuja
kutofautiana, kila mtu akaishi kivyake. Yakazungumzwa mengi kuhusu
chanzo cha ugomvi wao lakini pointi ya msingi ni kupishana kauli
kibinadamu kama watu wengine wanavyoweza kutofautiana na kupatana.
Kwa
upande wao suala la kupatana limekuwa zito, ugomvi wao haufiki tamati
huku kila kukicha ni malumbano ambayo yanawagawa mashabiki.
Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel wakipozi.
Tatizo
kubwa linalochagiza ugomvi wao ni mitandao ya kijamii, kumezuka makundi
ambayo yamekuwa yakitumia utabiri wao wanaoufahamu wenyewe kuzidi
kuchochea ugomvi uliokuwepo kati ya mastaa hawa wawili na wengine
wakitumia matusi mpaka ya nguoni kutukana wa upande wa Wema na Kajala.
Makundi
hayo ndiyo yamekuwa chachu kubwa ya bifu lao na kuzidisha mapambano
kati ya mastaa hawa ambao naamini wanapendana sana, sitaki kuamini
kabisa kama Wema hampendi Kajala, na sitaamini kama Kajala hampendi
Wema.
Staa wa filamu Bongo,Kajala Masanja.
Ndiyo
maana siku ambayo walipatana na kuzungumza kwa muda nyumbani kwa msanii
Aunt Ezekiel, mastaa hao walipata fursa ya kukaa pamoja na kuzungumza
baada ya ugomvi wao kila mmoja alitoa chozi kuonyesha jinsi gani kila
mmoja anaumia anapokuwa mbali na mwenzake.
“Mimi
nilikuwa napenda sana kukuangalia wewe na siyo timu zinazotuzunguka
zinazidi kututia chumvi tugombane, nakupenda na ninajua ni rafiki mwema
kwangu lakini unasikiliza sana maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala
niliyosikia akimwambia Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
Mastaa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja katika picha ya pamoja
Maneno
hayo waliyoambizana huku kila mmoja akitoa machozi, yalisahaulika kwa
siku tatu tu kwani viliibuka vitu ambavyo havikujulikana vilipotokea na
kuanzisha ugomvi mwingine mpya na kuwafanya wawili hawa kuvurugana tena
kwa kasi mpya na nguvu mpya.
Nathubutu
kusema kwamba ugomvi wa mastaa hawa mara nyingi unachagizwa na mitandao
ya kijamii. Hizi zinazojiita Team Wema na Team Kajala ndiyo tatizo
kubwa.Nasema ni tatizo kwa sababu hata ukiangalia kwa makini, kipindi
cha nyuma mastaa hawa walipokuwa wanaanzisha urafiki wao, timu hizo
hazikuwepo ndiyo maana waliweza kudumu.
Kwa
nini wanakubali kutawaliwa na hizi Team? Kwa nini waruhusu maisha yao
ya kila siku yaingiliwe uhuru wao wa kufanya mambo yao? Si sawa!
Mimi
naamini kabisa kama mastaa hawa wangekuwa na ugomvi wao bila hizi Team
kuingilia kati wangeweza kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao mapema
sana lakini tatizo kuna watu wa pembeni wenye kuzoa maneno huku na
kupeleka kule.
Kwa
jinsi ninavyoona mimi, hizi Team zikiendelea hivi na kwa mastaa
wengine, ipo siku watasababisha hata mauaji kwa jambo ambalo halina
kichwa wala miguu. Niwasihi Kajala na Wema wasijisahau kuwa wao ni
biashara, mashabiki wengi wanapenda kuona kazi zao, wangeweka tofauti
zao pembeni wafanye kazi na washirikiane hata kutengeneza filamu ya
pamoja.
Naamini
wakiweka pembeni hizi Team, wakaacha kusikiliza maneno ya kinafiki
yanayoundwa na baadhi ya wasanii wasiopenda urafiki wao, basi wataishi
vizuri na watafanya kazi zao pamoja!


