DIAMOND PLATNUMZ KUACHIA MPYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/diamond-platnumz-kuachia-mpya.html
Wakati
wimbo wa MdogoMdogo ukiwa bado unasumbua kwenye media, Diamond
Platinumz anatarajia kurusha mawe mengine mazito zaidi kwa ajili ya
kuwaburudisha mashabiki wake.
Babu
Tale ambaye ni meneja wa Diamond amesema mkali huyo anatarajia kuachia
nyimbo mbili kwa mpigo na kwamba zote zimetayarishwa nje.
“Tusubirie
kidogo, baada ya miezi miwili mitatu tutaongea kwa sababu kuna kazi
zinakuja, Diamond anarelease ngoma mbili mfululizo na zote zimetoka nje.
Lakini hatuwezi kueongea sasa hivi hadi muda ufike.”
Inaonekana
Diamond hataki kuacha gap, anakandamizia palepale azidi kwenda juu na
kutwaa tuzo nyingi za kimataifa kama alivyofanya mwaka huu.
