Diamond afunguka juu ya tofauti zilizokuwa zikizungumzwa baina yake na Alikiba
Diamond na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa za mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao,...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/diamond-afunguka-juu-ya-tofauti.html
Diamond
na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa za
mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao, Team Diamond
v/s Team Alikiba, ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo
Nasib Abdul amedai kuwa haipo.
Platnumz
ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka
juu ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa inazungumzwa baina yake na
muimbaji huyo wa ‘Mwana’.
“Nimekua
nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana, kwenye mitandao katika nini,
sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm
“Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu
sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni
msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo
yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu,
lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi
zako unazifanyaje ubora wake”.
“Tangia
mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo ilikua sijui kwa Belle 9,
ilitoka kwa Belle 9 ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja
sijui kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja
ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena
ikaja kwa Richard Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda unafanya
vizuri hivyo vitu vinakua vinatokea, so ni we mwenyewe kuangalia na watu
wasiokuwa na upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si
tatizo ni vitu ambavyo vitakuwepo tu kwasababu mashabiki wana tabia
wakiona mtu anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika kazi
inayofanana hivyo vitu vitatokea yaani watu watashindanisha, unaweza
hata ukashindanishwa na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.“Hata
kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East
Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye
mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga
ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”
Diamond
amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na tatizo na yeye anaamini angeweza
kumfata na kumwambia sababu amefahamiana nae kabla hajakuwa mwanamuziki.
“Sasa hivi yaani karibia mwaka wa tano, Mi
tangia nianze kufanya muziki sijawahi kudrop kila siku nazidi kupanda
juu…so hivyo vitu lazima vitatokea lazima nivikubali, inawezekana we
unasema we unasema we hauna tatizo lakini mwenzio akawa anahisi wewe una
tatizo nae, lakini naamini kama angekuwa anahisi kama mimi nina
matatizo na yeye angenifata akaniambia kwa sababu mimi sijajuana na Ali
kwenye muziki, nimejuana na Ali kabla sijakuwa mwanamuziki, nimemjua Ali
kupitia dada yangu Queen Darleen so alikuwa an uwezo wa kunifata
akaniambia personally kwamba bana umefanya hichi na hichi na hichi”.
Diamond
amemaliza kwa kusema kuwaomba media na mashabiki wasifanye ionekane
kama wana beef binafsi bali wazishindanishe kazi ili kukuza muziki wa
Tanzania.
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”