DAH!! RAFIKI YANGU" MAINDA AMLILIA SHERRY MAGARI
Staa wa Filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amemlilia rafiki yake kipenzi Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni na kusema...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/dah-rafiki-yangu-mainda-amlilia-sherry.html
Staa
wa Filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amemlilia rafiki yake kipenzi
Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni na kusema hana la kufanya
zaidi ya kumuombea.
Akizungumza
na Ijumaa juzi, Mainda alisema alikuwa amejipanga kwenda kumuona jana
‘Alhamisi’ baada ya kusikia kwamba hali yake haikuwa nzuri lakini ikawa
imeshindikana kwani kabla ya safari alipata taarifa za kifo chake.
“Nimeumia
sana tena sana, yaani dah! Amekwenda rafiki yangu, nilitamani sana
kumuona akiwa hai tuongee lakini Mungu akaamua kutenda kazi yake,”
alisema Mainda.
Marehemu Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni.
Sherry aliugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na kufikwa na mauti alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

