Breaking: Chid Benz kakamatwa na Polisi Airport
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/breaking-chid-benz-kakamatwa-na-polisi.html
Najua
kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na
twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza
kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid
Benz amekamatwa na Polisi.
Taarifa
zinasema kakamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa
anaelekea Mbeya na hiyo imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni
kosa kwa yeyote kukutwa navyo.
Wakati millardayo.com inaendelea
kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi, tumezungumza na
muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz ndio alikua
anakwenda kushiriki kesho.
Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu >>> “Sijapewa
taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es
Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba
haviruhusiwi kupita Airport“
Chidi
Benz alikua ameongozana na msanii mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi
kabaki na Polisi na Shetta amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea
Mbeya.
Source Millardayo